Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Saa 8:30 usiku wa kuamkia leo,Mjini Quito Ecuador,wenyeji Ecuador waliingia dimbani kumenyana na makamu bingwa wa dunia Argentina. Pambano la mwisho kufuzu au la kombe la dunia. Argentina ya Messi ilikuwa nafasi ya sita muda huo.
Kikosi cha Argentina,pamoja na kuwajumuisha Messi,Mascherano na Di Maria,hakikuwa na Dybala wala Higuain upfront. Hata Mauro Icardi hakuanza. Imani na matumaini ya Argentina yalibaki kwa Lionel Messi aka Andunje,the Captain.
Wenyeji Ecuador wakaanza mpira kwa kasi. Wakashambulia kwa nguvu. Sekunde ya 40 ya mchezo,Ecuador wakapata bao. Walishtua kila mtazamaji. Walitishia uwepo wa Argentina nchini Urusi kwenye kombe la dunia. Kiukweli,Argentina walianza mchezo kwa panic na stress. Hatimaye,wakatulia.
Ndani ya dakika 20 kuanzia hapo,Messi akapiga mabao mawili. Akapindua matokeo na kurejesha matumaini ya nchi yake kufuzu. Dakika ya 63 kipindi cha pili Messi akamaliza kazi kwa kufunga bao la tatu. Messi alipiga mpira mkubwa. Kocha Jorge Sampaoli alitulia. Mambo yakawa mambo.
Argentina ya Messi imefuzu nyuma ya Brazil,Uruguay na Colombia. Peru atasaka tiketi kwa New Zealand.TeamMessi/Argentina mko wapi tupongezane kwa kula na kunywa? Vile ndivyo tegemeo wanavyotegemeka na kubeba timu au taifa lake!