TeamMessi/Argentina niwakute wapi tule na tunywe kwa furaha?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Saa 8:30 usiku wa kuamkia leo,Mjini Quito Ecuador,wenyeji Ecuador waliingia dimbani kumenyana na makamu bingwa wa dunia Argentina. Pambano la mwisho kufuzu au la kombe la dunia. Argentina ya Messi ilikuwa nafasi ya sita muda huo.

Kikosi cha Argentina,pamoja na kuwajumuisha Messi,Mascherano na Di Maria,hakikuwa na Dybala wala Higuain upfront. Hata Mauro Icardi hakuanza. Imani na matumaini ya Argentina yalibaki kwa Lionel Messi aka Andunje,the Captain.

Wenyeji Ecuador wakaanza mpira kwa kasi. Wakashambulia kwa nguvu. Sekunde ya 40 ya mchezo,Ecuador wakapata bao. Walishtua kila mtazamaji. Walitishia uwepo wa Argentina nchini Urusi kwenye kombe la dunia. Kiukweli,Argentina walianza mchezo kwa panic na stress. Hatimaye,wakatulia.

Ndani ya dakika 20 kuanzia hapo,Messi akapiga mabao mawili. Akapindua matokeo na kurejesha matumaini ya nchi yake kufuzu. Dakika ya 63 kipindi cha pili Messi akamaliza kazi kwa kufunga bao la tatu. Messi alipiga mpira mkubwa. Kocha Jorge Sampaoli alitulia. Mambo yakawa mambo.

Argentina ya Messi imefuzu nyuma ya Brazil,Uruguay na Colombia. Peru atasaka tiketi kwa New Zealand.TeamMessi/Argentina mko wapi tupongezane kwa kula na kunywa? Vile ndivyo tegemeo wanavyotegemeka na kubeba timu au taifa lake!
 
On behalf of all Messi fans worldwide, I want to say a very big thank you to all the well wishers and and also the haters who stayed up all night to see the Greatest player of All time prove himself ones again..

See you at Russia
 
The greatest player of all time The King Messi.


Narudia tena na tena. Messi hafananishwi na vitu vya kijinga.

Tokea soka lianzishwe adi leo hii 2nazungumza cjaona wa kumfikia Huyu kiumbe kuwahi kutokea.


Shikamoo KING MESSI

Shikamoo THE PLAYERS OF ALBICELESTE___The great/best team in the world iliosheheni wachezaji bora kuwahi kutokea ktk tim.
 
Hajabeba world cup na timu yake ya Taifa hivyo hafuzu kuitwa mchezaji bora wa muda wote - By G. Infantino
 
Reactions: BAK
Mnashabikia kufuzu? Nilifikiri kachukua kombe kama yule mwingine yaan CR7
 
Na kwa mpira waliocheza jana kama hakutakuwa na
improvement na wapangwe kwenye kundi gumu basi watafungishwa virago raundi ya kwanza. Naunga mkono hoja yako.

Hajabeba world cup na timu yake ya Taifa hivyo hafuzu kuitwa mchezaji bora wa muda wote - By G. Infantino
 

Nipo katika jiji la Buenos Aires pembezoni mwa bahari napata redbull
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…