TEC, BAKWATA na CCT saidieni kuinusuru Nchi hii.

TEC, BAKWATA na CCT saidieni kuinusuru Nchi hii.

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika jana ni hatari tupu. Mambo ya ovyo yalifanyika wakati wa uandikishaji, uchukuaji fomu za kugombea, urudishaji fomu, uapishaji mawakala, kabla, wakati na baada ya uchaguzi ni viini macho vitupu.

Ndugu zangu viongozi wa Dini, nafikiri sasa ni wakati wa kuongoza mapambano ya kuirejesha haki na amani vinavyozidi kupotezwa na wenye Mamlaka. Kwa sasa hakuna msaada zaidi ya ninyi viongozi wetu wa Dini.

Bunge lipo mikononi mwa mtu mmoja, Mahakama vile vile, vyombo vya ulinzi na usalama vipo mikononi mwa mtu mmoja.

Katika hali hiyo, Watanzania watakimbilia wapi? Nani atawasaidia? Wanaotakiwa kuwalinda na kuwatetea Watanzania wote wapo mikononi mwa mtesaji.

Ebu fikirini, vyama vya upinzani walivyoweka Wagombea wao lakini wanafanyiwa mchezo wa ovyo kabisa.

Kusimamisha mgombea, kupiga kampeni na mengineyo ni gharama kubwa sana. Lakini wenye Mamlaka wanathubutu hawajali hata kidogo.

Ndugu zangu viongozi wa Dini, naomba mshike usukani, mtuongoze sisi waumini kuirejesha haki na amani vinavyozidi kupotezwa na wenye Mamlaka. Mtuongoze nini kifanyike ili kuepukana na LAANA inayolinyemelea Taifa letu.

Ingekuwa Mahakama zipo, watu wangepata haki mahakamani. Ingekuwa kuna Bunge la Watanzania, wabunge wangedai haki hiyo.

Hili linatuhusu sisi sote, asipatikane mtu wa kudhani kwamba halimhusu.

Mimi napendekeza, kila tunapokutana kwenye Ibada zetu, mwishoni mwa Ibada zitumike angalau dakika 10 hivi kuelezea hali hii. Hii itawasaidia watu kujua wajibu na haki zao. Tuelezee hasara ya kuwa na utawala wa mtindo huu.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania. Amina.
 
Back
Top Bottom