- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimekutana na hii Taarifa kwa Umma je ni kwelli imetoka TEC?
- Tunachokijua
- Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) ni baraza la maaskofu wa katoliki nchini Tanzania abalo lilianzishwa rasmi mwaka 1956 na kutambuliwa na seikali mwaka 1957.
Madai
Julai 04, 2025 kumeibuka barua yenye utambulisho wa baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) ikiwa na ujumbe wenye kichwa kinachosomeka “JUMAPILI NI YA IBADA SIO MAANDAMANO YA UCHOCHEZI”.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si kweli.
Taarifa hiyo kwa umma ni ya kughushi kwani haijatolewa na baraza la Maaskofu Tanzania (TEC). Taarifa hiyo imetumia aina tofauti ya mwandiko (font) tofauti na inayotumiwa na baraza hilo. Aidha taarifa hiyo ina mpangilio tofauti na barua zilizowahi kutolewa hapo awali na baraza hilo.
Ufuatiliaji umebaini pia hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo. Juni 29, 2025 Rais wa TEC, Askofu Wolfgang Pisa aliitangaza Agosti 23, 2025 kuwa ni siku ya kuombea haki na Amani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.