Justdr
Member
- Jun 1, 2021
- 52
- 104
Mwanateknolojia wa kibaolojia na mtayarishaji wa Filamu Hashem Al-Ghaili anatupeleka kwenye ziara isiyotulia lakini ya kuvutia ndani ya EctoLife - kituo cha kwanza cha uzazi wa mpango
EctoLife ni teknolojia itakayowapa wazazi wa siku za usoni njia mbadala inayodhaniwa kuwa salama zaidi ya uzazi wa asili, kuondoa matatizo ambayo mara nyingi huwa hatari yanayohusiana na uzazi.
Mfano kifurushi cha "Elite package" kitaruhusu watu kuchagua kiwango cha akili cha mtoto wao, urefu, nywele, rangi ya macho, nguvu za mwili na hata rangi ya ngozi.
'Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, karibu wanawake 300,000 wanakufa kutokana na matatizo ya ujauzito.
Tumbo la uzazi la EctoLife limeundwa ili kupunguza mateso ya binadamu na kupunguza uwezekano wa kujifungua kwa upasuaji,' anaandika Al-Ghaili.
Badala ya mama kusukuma kwa uchungu na mwili wake, wanandoa wanatakuwa wanabonyeza kitufe ambacho kitawapa mtoto wao aliyepachikwa. Mradi huo pia umeundwa kwa ajili ya wanawake ambao wameondolewa mfuko wa uzazi kufuatia maswala ya kiafya, kama saratani,nk.
Al-Ghaili anaamini kwamba vifaa vya mfuko wa uzazi bandia vinaweza kuwa tiyari kabisa katika miaka 10 au zaidi ikiwa vizuizi vya maadili vitaondolewa.
"Kila kipengele kimoja kilichotajwa katika dhana kimekamilika na ni asilimia 100 ya sayansi na tayari kimefikiwa na wanasayansi na wahandisi", alisema.
"Kitu pekee kilichosalia ni kuunda mfano kwa kuchanganya vipengele vyote kwenye kifaa kimoja", mtengenezaji wa filamu alinukuliwa akisema.
Anasema mara tu vikwazo vya kimaadili vinapolegezwa, watu wanaweza kuwa tayari kutumia teknolojia hiyo katika siku za usoni.
Je, Wataalam wanasema nini?
Wataalamu wanaamini kuwa teknolojia hiyo sio ya mbali sana na inaweza kuwa ukweli katika siku zijazo. Andrew Shennan, profesa wa Uzazi katika Chuo cha King's London, aliiambia HuffPost, "Kwa mtazamo wa kinadharia inawezekana. Ni suala la kutoa mazingira sahihi na oksijeni na teknolojia zipo ili kuweza kufanikisha hilo.