GE2025 Tecla Ungele ajitosa tena ubunge viti maalum Mkoa wa Lindi

GE2025 Tecla Ungele ajitosa tena ubunge viti maalum Mkoa wa Lindi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Lindi Tecla Ungele ni miongoni mwa waliochukua fomu leo Juni 30,2025 za kuwania tena nafasi hiyo.

Tecla amechukua fomu hiyo katika Ofisi za Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Lindi na kukabidhiwa na Katibu wa Umoja huo wa Mkoa Ndugu Neema Ngonyani.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo amesema ameamua kujitokeza kuwania tena nafasi hiyo ili kuendelea kufanya kazi na wananchi wa Lindi wakiwemo wanawake na Watoto wenye mahitaji maalumu pamoja na kuendelea kushirikiana na maafisa maendeleo ya jamii katika kuhakikisha wanawake wanainuka kiuchumi.
1751287089011.jpeg
 
Back
Top Bottom