TECNO kuachia toleo jipya la simujanja TECNO CAMON 18

TECNO kuachia toleo jipya la simujanja TECNO CAMON 18

TECNO Tanzania

Senior Member
Joined
Jul 6, 2016
Posts
192
Reaction score
217
TECNO tunatarajia kuachia toleo jipya ya simu janja TECNO CAMON 18 hivi karibuni ambayo italeta ushindani mkubwa na simu kutoka kampuni ya Samsung. CAMON 18 Premier ina sifa kuizidi simu ya Samsung Galaxy A52.

Picha 1.jpg



Kamera
TECNO CAMON 18 Premier ina sifa ya kipekee kuwa na GIMBAL CAMERA, ambayo itamsaidia kuchukua video kali na thabiti bila kutikisika., tofauti na simu ya Samsung Galaxy A52 ambayo haina sifa hiyo.

Betri na Uwezo wa Kuchaji
Kwa upande wa kuchaji simu TECNO CAMON 18 Premier imeongoza ambayo ina betri ya 4750mAh inaweza kujaa chaji kwa haraka kutokana na kuwa simu hii inakuja na teknolojia ya Fast charging ya hadi 33 W.
Tofauti na Samsung Galaxy A52 simu hii inakuja na battery ya 4700 mAh, ambayo ina 25 W

KIOO
Tukianzia kwenye upande wa kioo au display, TECNO CAMON 18 Premier pia inaongoza inakuja na kioo cha inch 6.7 tofauti na simu ya Galaxy A52 yenyewe inakuja na kioo cha inch 6.5.
Mbali na hayo simu ya TECNO CAMON 18 Premier ina kioo cha AMOLED chenye refresh rate ya 120Hz kubwa zaidi ya Samsung Galaxy A52.

STORAGE (Rom)
Kwa upande wa uhifadhi wa ndani au ROM, TECNO CAMON 18 Premier inakuja uhifadhi wa 256GB, tofauti na Samsung Galaxy A52 ina uhifadhi wa 128GB.

Picha 2.png



Ram
Kwa upande wa RAM ni wazi kuwa simu hizi zinalingana zote zikiwa na RAM ya GB 8, hapa lakini kwa upande wa TECNO CAMON 18 Premier unapata toleo lenye GB 8 za RAM huku kwa Samsung Galaxy A52 ukiwa unapata matoleo ya GB 4, 6 na 8.

Bei na upatikanaji
Mpaka sasa tetesi zinasema zimu hiyo itakuwa inapatikana kuanzia Tsh 790,000/= ambayo ni bei rahisi sana ukilinganisha na sifa ambazo simu hiyo ipo nayo. Tofauti na simu ya Samsung Galaxy A52 ambayo inapatikana kwa Tsh 1,000,000/=.

Kujua zaidi tembelea: Home-tz-坦桑尼亚-斯瓦西里语
 
Moja ya tangazo bovu la simu kuwahi kuliona, tukiachana na Mambo ya ubora Kama camera, ram na vingine, kampuni kubwa huwezi kutangaza bidhaa yako at the same time unaiponda bidhaa ya mshindani wako, hivi ushawahi kuona tangazo la Coca akimponda Pepsi au Pepsi akimponda Coca?
 
Moja ya tangazo bovu la simu kuwahi kuliona, tukiachana na Mambo ya ubora Kama camera, ram na vingine, kampuni kubwa huwezi kutangaza bidhaa ya yako at the same time unaiponda bidhaa ya mshindani wako, hivi ushawahi kuona tangazo la Coca akimponda Pepsi au Pepsi akimponda Coca?
So unprofessional...
 
Moja ya tangazo bovu la simu kuwahi kuliona, tukiachana na Mambo ya ubora Kama camera, ram na vingine, kampuni kubwa huwezi kutangaza bidhaa ya yako at the same time unaiponda bidhaa ya mshindani wako, hivi ushawahi kuona tangazo la Coca akimponda Pepsi au Pepsi akimponda Coca?
Hata mimi nimeshangaa sana. Huyu admin. wa hii akaunti ya TECNO ni boya kama zilivyo simu zao za TECNO.
 
Yaani mnafanya mashindano? Napenda camera za Techno ila sio kwa ulinganisho huu
 
Admin kapigwa Spana mpaka kaenda kulia kwa mod wambadilishie title ya thread yake.

Nyinyi watu wa tecno ni wa hovyo kama zilivyo simu zenu.
 
Back
Top Bottom