Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Service charge inarudi hiyooooooo..

Ova
 
Watanzania bwana, yaani watu wengi kumbe uwa awafuatilii habari kwa kina ushabiki tu na thread zinapita hapa hapa JF.

Hili swala TANESCO mbona walishajikinga, ikitokea wakishindwa hii kesi PAP ndio walipe deni na ndio kigezo cha mahakama pia kabla ya malipo kutolewa.

Hoja za msingi tunatakiwa kujiuliza third party rights kwenye mkataba, exclusiveness na mantiki ya sheria zetu. Maana TANESCO hawana mkataba na HSC huu ni ukoloni mambo leo tunao ushangilia.
 
hahahahaaa na bado mtaisoma namba
kuisoma namba kwangu inamaanisha kwamba Sisiemu lazika ishinde uchaguzi kwa bao la mkono ili watanzania waendelee kunyonya ili bills kama hizi za dowans,iptl zilipwe zote sasa nani mwingine wa kulipa ikija regime nyingine itakuwa hatari tupu
 
Unapewa kazi yakusimamia rasilimali za wanyonge unaishia kuliingiza taifa kwenye mitego ya kulifirisi.
Mabilioni ya escrow yalitoka fast a bila hata kutafakari kdog. Bado vidonda havijaisha Mengine tena hayo. Tukisema turudie kujadili wazee wa makofi watasema sioooooo.
 
Cheki akili za mtu huyu hatutoboi kama tutaendelea kuwaombea watu ili watuibie sasa sijui na wewe ni mnufaika makitu hii.




Jaribu kuwa na akili japo kidogo,mabilioni hayo ya shilingi yanayodaiwa ndiyo yale ambayo vigogo waandamizi wa chama na serikali yako tukufu waligawana na kuyapakia kwenye mifuko ya Rambo pale Stanbic Bank,hao wapambe wako unaowaabudu kama ni wazalendo kwa nini hawawakamati waliogawana mabilioni hayo na kuyabeba kwenye viroba?

Miezi 11 tangu waingie madarakani wanashindwa nini kuwataja wale wote waliohusika na sakata la Tegeta Escrow?Wanashindwa nini,au mabilioni hayo yalitumika katika kuwaweka madarakani?
 
pesa imelipwa kwa watu waliokuwa wakiendesha mradi,really people hawa hongkong bank wanatokea wapi,maana hatukununua umeme toka standard chartered hongkong,
kama yule singa alikopa hela huko akawazunguka watajijua wenyewe,sisi tumelipa watu waliokuwa field,wakiendesha mitambo na kutuuzia umeme ambao tuliutumia
 
Kama walijikinga, kwa nini walipeleka kesi mahakamani in the first place na kulipa legal fees kubwa tu, kwani at the end of the day hawatakalipa chochote???
 
hii nchi ilishalaaniwa hakuna fedha

Tanzania haijalaaniwa na haitalaaniwa.Wezi wamelaaniwa isipokuwa wakiomba toba.Waliotufikisha hapa kwenye IPTL inatakiwa tuache ujinga wa kujadiiana kwa mtazamo wa vyama.Waliotusababishia kero hizi hata kama ni rafiki zetu tushinikize wachukuliwe hatua wanazostahili.Tuache ujinga wa kutaka "wangepelekwa mahakamani" haya sasa mahakama za kimataifa zieama,je ina tija kwetu? huu ndiyo utawala wa sheria tunaoulilia.

Sheria inategemea mtawala alitaka ilinde nini na kwa maslahi ya nani.Adhabu hii ya kipuuzi ni kwetu sote watanzania.Tumeumia.
 
Kalasinga ni mtu wa kupull string behind the scene!katupatia kweli
nilipigia mistari eneo la rweyongeza advocates firm
 
hao wanasheria wetu wafatiliwe kwa karibu sio bure wamehongwa kujikosesha kwenye hii kesi
 
Pia wote waliohusika kudanganya Bunge na wananchi kwa ujumla washitakiwe na Sheria ichukue mkondo wake...walisema pesa sio ya serikali wala sio ya Tannesco kama nakumbuka vizuri
Kwa serikali ipi mkuu?Ambayo itachukua hatua hizo..
 
Kwahiyo hapo sisi watumiaji ndo imekula kwetu nchi hii ina mambo ya kijinga sana na hili shirika sijui kwanini wanashindwa kulipa mshindani wake kama ilivyo mitandao ya simu mana lingeshajifia siku nyingi huduma mbovu ila maingizo yao makubwa

Hiki ndicho kinapelekea watanzania kuendelea kusoteshwa mazima. Kwa mawazo na akili yako unafikiri shirika linashindwa kufanya kazi ama wafanyakazi au viongozi ni dhaifu? Hujajua tu tatizo liko wapi pamoja na mambo yote yalivyo wazi nyakati hizi! Serikali isipoamua kuweka sawa maswala yote yanayohusiana na umeme na mikataba yake unafikiri kuna dawa?
 
Kwa mawakili wetu hawa wa serikali? Lazima tushindwe kila siku.
 
Maamuzi ya kisheria ndio yameishatoka sasa nyie endeleeni kuruka "samba soti".
so unawaamini sana hao wazungu na mahakama yao fake?,
hao ni international conmen ,mkiwalegezea mtauza hadi nguo za ndani kuwalipa,na ikishaa hiyo utasikia kumbe standard chartered hongkong nao waliuza deni kwa swiss bank ambao nao wamefungua kesi ya madai dhidi ya Tanesco,mtakamuliwa mpaka basi..
Ilimu ilimu ilimu
 
Ha ha hah! Law firms chali. Kweli au kuna...

Something smelling fishy
 

Na serikali inaenda kuangukia pua.
 
Kesi zingine wamuombe Lissu na Kibatala wakapambane kwa manufaa ya taifa.
 
Bunge liliazimia serikali isiendelee kulipa IPTL na ile mitambo itaifishwe kwa nn hili halijufanyika??
Bunge ni ''Toothless dragon"hana uwezo wa kumwajibisha serikali japo sheria imempa mamlaka hayo ila kiutendaji ni mbwa asiye na meno hang'ati ndipo sasa unakuta anatoa maazimio yasio na tija yoyote kiutekelezaji.
 
Tulipo fikia kwa sasa wakamue tu tena sana, ili adabu irudi kwa raia wa vijijini waelewe nini mana ya siasa uchwara. Sio kupelekwa pelekwa kwa ulaghai wa kanga na kofia then maisha yanaishia hapo.
Haiwezekani watu wachache wabebe "mboneka" kwenye sandarusi na viroba, huku wengine wakitamba zilikua hela za mboga tu, na bado serikali inakenua meno.
Ndio hapa tuone kipimo cha jeuri na utumiaji nguvu ulipo.
Wakamue tu, tena kamua sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…