Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Kama walijikinga, kwa nini walipeleka kesi mahakamani in the first place na kulipa legal fees kubwa tu, kwani at the end of the day hawatakalipa chochote???
Kumbuka as far as TANESCO is concerned wao wanamkataba wa kuzalishiwa umeme na IPTL.

How the ownership of IPTL changes hand sio tatizo lao; kwa hivyo mzozo wa umiliki ni shida ya PAP na Standard charter. Mahakama yetu imemtambua PAP kama ndio mmiliki halali wa IPTL baada ya kumaliza mgogoro wa umiliki na mmbia mmoja anayetambulika na BRELLA ambaye alikuwa Rugemalira.

Hao wazungu wamenunua tu deni la IPTL lakini awataki tena kulipwa hela tu bali wanataka umiliki wa IPTL na wanadai wao ndio wamiliki halali. Huko sasa kwenye umiliki TANESCO ausiki.

Na malipo ya escrow yametolewa baada ya mahakama kuamua mmiliki ni PAP kwa hivyo TANESCO wala mwanasheria mkuu aliye hukumiwa awakuwa na jinsi maana sheria ishasema. Walichotaka TANESCO mahakama itambue kama ulinzi wao akija mwingine kudai na yeye ndiye mmiliki wa IPTL waende kudaiana mahakamani ndio ilikuwa kigezo chao cha kutolewa hiyo hela na mahakama ikaridhia hivyo.

Halafu hiyo habari yenyewe imeandikwa kwa bias ya upande mmoja, kitu kinacho encourage na kuwapa nguvu hawa standard charter ni ushabiki wetu wenyewe uliojaa ignorance its simple kampuni bado ipo kwanini wasidai deni walilonunua wao awataki malipo ya deni bali wanataka kampuni na kuna watu wanawatetea amazing: only in Tanzania
 
hii nchi ilishalaaniwa hakuna fedha
Ndio hivyo mkuu yaani hii ni sawa na mzazi anashindwa kufanya maamuzi ya kununua fridge familia yake ijidai kwa kunywa maji ya baridi kipindi cha joto, lakini kila mwaka inakuwa inalipa fidia na madeni kwa kuharibu mali za wengine. Kila mtu na mnyonge wake, serikali inatulalia sisi hasa tunapopatwa na majanga hata kama umekata bima watatafuta weakness point ili mradi uonekane mtumiaji umeme mzembe na nyumba imeungua kwa uzembe wako wakati wao kila siku wanalipa faini na wana timu ya wasomi. Ngoja tuhamie Mobisol tukapate solar za mkopo zenye mwanga wa kutosha na deni likilipwa tutarudi kutumia umeme wa TANESCO
 
Naona kama bill ya umeme kupanda ghafla
Na mkataba TANESCO na Ewura mwaka huu mwishoni TANESCO wanatakiwa kushusha bei ya umeme kwa 7%. Kwahiyo hawana ataa ajaa ya kupandisha bei ,ni uamuzi Wa kimya kimya tuu Tanesco awatapunguza bei .
 
Unajua ukikufuru kwa Mungu majaribu yatakuwa mengi mpaka utubu!!
Haya yule mtakatifu asiye jaribiwa aseme sasa!! Ni nani aliyemjaribu! je ni upinzani? Kama hatachukua hatua tutamuelewa kama mbaguzi mtumbuaji!!
 
Mnatamani sana Serikali ipandishe bei ya umeme ili muwe na ajenda majukwaani. Mmeula wa chuya. Hilo halitarokea kwa utawala wa Rais Magufuli
Wapandishe au wataacha tuu.kushusha bei kwa 7% mwishoni mwa Mwaka huu .kama ambavyo mkataba uliopo baina tanesco na ewura unavyotaka !!?? Ccm mnafikiri atujui hiloo ?
 
Ka uchumi kenyew na hilo Deni + Deni LA Taifa
Dah hii awamu tata sana
[emoji123] [emoji119] [emoji120]
 
Kwa nn watu hatuna uzalendo kazi kuombea mabaya tu serikali why,inawezekana kabisa nyie mnaoombea mabaya hata familia zenu huwa mwaziombea mabaya iweni na uzalendo
Tumeombea mabaya watu wabebe pesa na sandarusi kutoka benk.Tumeombea serikali imlipe Singh pesa isiyo yake.tumeombea tudaiwe bilioni 300 .tumeombea mawakili Wa tanesco washindwa kesi !!!!!????
 
Hivi mnajua walioanzisha IPTL mpaka akizaliwa kitu inaitwa escrow mwanzilishi wake ninani kama sio hao waliokuwa wakiitwa boys 2man?
 
Fuluuu uchocheza kwa mheshimiwa huu.[emoji1] [emoji1] [emoji1][emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Hapa pia Mahakama zinaichanganya TANESCO- Mahakama yetu iliipa PAP UMILIKI baada ya kuwa imemalizazana na Rugemarila kuwa ndo mmiliki halali wa IPTL, Bahati mbaya TANESCO wakawa washailipa PAP pesa yote bila hata kusubiri kesi yao walioshinda kwenye capacity charge.
Leo hii ICSID ime rule out kuwa mmilikiwa IPTL ni standard SBC-HK, kwakuwa TANESCO washaomlipa pesa zote PAP, kwanini PAP asirudishe hizo hele akapewa SCB-HK, kwanii TANESCO ilipe tena wakati ilishalipa? sijaliona tatizo la TANESCO-Mambo nani mmiliki wa IPTL hayaihusu TANESCO. Makosa makubwa ya TANESCO ni mawili. i kuwahi kulipipa PAP kabla hata ya kusubiri hukumu juu ya capacity charge na la pili ii. Kutosubiria mgogoro wa umiliki wa IPTL iliijue exactly inamlipa mmiliki halali
 
Nataka kujua IPTL ni nani? nani mwanzilishi wa hii company? maana tunaelewa IPTL= 30% VIP (Kamanda rugemalila)+ 70% IPTL ( ambao hawajulikani), inakuaje tunatambua tu 30% ya umiliki wa share ya VIP na hatumtambui mweye 70%? tukishamtambua mmiliki halali wa IPTL ndo tutajua picha kamili ya huu ufisadi, maana hatuwezi tu kusema PAP ni mmiliki halali aliyenunua IPTL baada ya wabia hao kupatana, na mahakama ya Zimamoto ya Tanzania haimtaji IPTL inamilikiwa na nani?, inawezekana IPTL mwenye 70% ndo huyo huyo PAP anachofanya anabadili jina tu, bure kabisa.
 
Maazimio ya bunge kuhusu ESCROW mpaka leo serikali haija yafanyia kazi. TUTAPIGWA SANA.
 
IPTL inaonyesha kwa Mara ya kwanza iliingia nchini mwaka 1994 wakati huo Rais akiwa Mwinyi!!
Ikaendelea kwa Mkapa ingawa imekuja kuanza kuwa Kansa ndani ya utawala wa Kikwete!!

Walionyuma ya IPTL ni watu wengi sana ila nashauri Rais Magufuli angewahoji
Marais wastaafu kwanza
Mawaziri wakuu waliopita
Mawaziri wa nishati waliopita
Mawaziri wa fedha waliopita
Wanasheria wakuu wa Serikali waliopita!!
Na magavana wa benki kuu waliopita !!

Bila kufukua makaburi tutaendelea kusubiri sana!!
Hii kitu inaonyesha kikwete alikuwa waziri wa nisharti mwaka 1994 na hapo ndipo tuanzie!!
 
Maazimio ya bunge kuhusu ESCROW mpaka leo serikali haija yafanyia kazi. TUTAPIGWA SANA.
Hivi inakuwaje kiutaratibu pale serikali inapokaidi maamuzi ya bunge Kwa nchi zinazoheshimu taratibu kanuni na sheria anyway
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…