Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

TZ ina vyanzo vingi vya mapato tunaweza lipa tena kwa mkupuo kama tulivyonunua ndege:
1. Kuongeza malipo ya mikopo ya wanachuo.
2. kufuta fao la kujitoa
3. Kufuta kiinua mgongo kwa wastaafu.
4. Kuongeza makato kwenye miamala ya benki
5. Kuongeza makato kwenye simu
 
Hivi bajeti ya wizara ya viwanda ni bei gani vile...ukilinganisha na hii pesa??
 
IPTL ukiwaangalia vizuri Nchi za kusini wapo Tanzania tuu ni kuchaka cha kupigia hela za Tanesco, bill zipo juu kwa sababu ya hawa wachache na sisi tupo kimya tuu..
Hii ni nchi ya amani zanzibar na bara. ACHA UCHOCHEZI. Ukileta fyokofyoko majeshi yataanza kufanya usafi sasa hivi
 
Mkuu hayo unayoyasema ni kweli yanaingia akilini. Sie tunapata umeme (hata kama bei ni kubwa[emoji15] ) umiliki hautuhusu sawa.

Sasa cha kujiuliza baada ya hukumu na pesa kutolewa kwa PAP na ruge iweje kwenye mgao huo$$$

wapewe majaji (hukumu ilikuwa ya haki?

Watumishi waandamizi wa serikali akiwemo aliyekuwa mwanasheria mkuu na aliyekuwa waziri wa nishati?

Hii inaingia akilini kweli, kwa nini watu walichota fedha sitaniibenki haraka haraka kwa magunia na mabilioni kinyume cha taratibu za ki benki? Huu sio wizi kweli?

Tumerogwa au
 
"Uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi kubwa sana, Tanzania ya viwanda inakuja sasa, wanaosema hakuna pesa walizoea kupata pesa za kifisadi, Mapato ya bandari yameongeza maradufu, msinijaribu!"

[HASHTAG]#HAPA[/HASHTAG] KAZI TU!
 
Wewe ulisikia wapi dunia watu wanagawana pesa kwenye visalphate, magunia na mafuso? Matokeo yake ndio haya sasa. Serikali inatakiwa kulipa kwa sababu ndio walioweka dhamana. Only in Tanzania. Wacha tu tuisome namba.
 
Nimesikitishwa sana na habari kuwa Tanesco wameshindwa kesi ya IPTL na inartakiwa kulipa $148 milion.

Naomba niulize Ndugu zangu wenye kumbukumbu nzuri, Mbona kesi nyingi sana zinazofunguliwa na Jamhuri Hazizai matunda?????

1. Ni mahakimu?
2. Ni mawakili?
3. Ni Rushwa?
4. ............................?

Hii serikali si inatumia maqkampuni binafsi kuendesha kesi au inatumia mawakili wake?
 
Hivi serikali yetu imewahi kushinda kesi[emoji41][emoji57] nauliza tu.
 
Wakishalipwa hao watakuja MECHMAR nao kudai.......na deni la taifa litazidi kupungua according to Dr Ndulu
 
TANESCO imekamatika tena. Inapaswa kuwalipa Standard Chartered bilioni 320. Haina jinsi ya kufanya,zaidi ya kulipa. Kashfa inayokera ya Escrow imeibuka tena. Imekuja kivingine!

Wakati wa kashfa ya Escrow ambapo mabilioni yalichotwa,kubebwa na kulipwa kwa watu mbalimbali kulikuwa na malumbano ya hoja yasiyo na tija wala haja. Malumbano yalikuwa: ni fedha za umma au si za umma?

Watawala walisema si za umma. Watawaliwa wakasema ni za umma. Mjadala ukalala. Waliopata wakapata,waliokosa wakadata. Kwa deni hili jipya kwa TANESCO la bilioni 420,tuendelee na malumbano yetu?

Mimi nawakera tena,TANESCO haitalipa deni hili kwa fedha za umma!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Namuona Mheshiwa "wapigwe tu" kwa mbaaalii........AKITABASAMU BAADA YA KUTUMWA NA CCM NA KUFANIKIWA KUWADANGANYA WATZ ILI WAGAWANE PESA NA BAADAYE WATZ HAOHAO WABEBESHWE MZIGO WA KULIPA.....
Tanzania Shamba la bibi kizee
 
Wamemwacha Mkono Law Firm, wacha waendelee kupigwa tu mahakama za kimataifa. Walikuwa wanafikiri ni Kisutu wanakopangana mahakimu na mawakili kupiga madili.
 
Kwani Tane
Walifunika-funika moshi , leo hamadi moto unawaka [emoji91] [emoji91]

Kwa mbali namuona Kafulila "the monkey trouble" [emoji87] yuko juu anatazama watanzania walivyo wajinga tumepigwa teena.
Tanesco isipolipa hakuna shida. IPTL hawana uwezo wa kucheza na dola. Watafanya nini? Hakuna kitu. Dawa ni kutolipa tuone watakachofanya hao IPTL.
 
Tulimtukana David Kafulila,tukamwita majina yote,leo ukweli uko sebuleni.Baba Taulo limedondoka.Waliochota hizo pesa ndiyo walipe.Waziri Muhongo sijui leo atatuambia nini!

Mwache Profesa wetu. Yeye aliletewa mwekezaji na wanasheria wakamthibitishia kuwa sheria zote zimefuatwa. Jaji akasema pesa zilipwe na zikalipwa kwa matapeli, majaji, mawaziri, wabunge na hata maaskofu. Mamlaka za juu zikasema pesa ni za wenyewe na wenyewe siyo TANESCO. Nina hakika profesa hakupewa hata za chai acha za mboga! Hapa tunataka kuona mamlaka mpya zitaita beleshi (spade) ni beleshi au ni kijiko kikubwa!!!!!!!!
 
Waliokwapua hizo hela ndio viongoI wako wa sasa,usitegemee wakusaidie zaidi ya kukubana na kodi kila kona. Kuna mmoja alisema bilioni 1.5 ni hela ya mboga.

Serikali hii ishughulikie tatizo hilo? Jamaa hana habari kuwa mtukufu keshaahidi kuwalinda wenye madili hayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…