Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Kwa kuwa mtaalamu wa kutumbua majipu tunaye, basi hata jipu hili linalotoa usaha sasa anaipata harufu yake! Atachukua hatua stahiki, In sha Allah!
 
Nilishajiuliza sana kuwa sote tuko hapa na uwezo wetu wa kufikiri sote tunajuana, sasa inakuwaje mmoja wetu, marafiki na familia yake wanatokea na kuanzisha 'foundations' zinazotoa mabilioni ya pesa mchana na usiku!?
Hapa ndipo napata jibu kuwa njia za haya mabillion ni nyingi na tukija kuziweka hadharani kuna watu tutagundua kuwa heshima na shikamoo tunazowapa ni kujidhalilisha!
 
Subiri uone kitakacho fuata:

Lilipoanza sakata la escrow nilisema ni hela binafsi sio za umma.

Walipotoa azimio la bunge nilisema alitekezeleki kisheria na Zitto aache cheap popularity kama ana amini inawezekana kisheria aende mahakamani.

Walipoitwa watu kwenye kamati ya maadili nilisema hakuna hatua za makosa ya jinai labda ethics

Waliofungwa nilisema wameonewa

Na hapa nakwambia hakuna hela TANESCO wala serikari italipa subiri uone.

Heck from December nilisema baadae mzunguko wa hela itakua shida serikari isipo invest hizi hela inazobana.

In short record yangu mwenyewe aijawi shindwa sio kwamba mganga elimu ina principles zake ukizijua you know what will follow given the variables and approach.

Na hapa subiri serikari aitolipa deni.
 
Kwa kuwa mtaalamu wa kutumbua majipu tunaye, basi hata jipu hili linalotoa usaha sasa anaipata harufu yake! Atachukua hatua stahiki, In sha Allah!
Wewe endelea kuota siku ukiamka unaambiwa ulipe laki tano kama gharama ya umeme ya mwezi
 


duh!

yani kosa lishakuwa la Tanesco?
 
Watashinda kesi vipi wakati hizo kesi wanatengeneza wenyewe na mahakama zenyewe zinakutana hotelini? CCM wakisha chacha lazima "Mahakama ya Migogoro ya Matapeli" inaamua TANESCO walipe hiki au walipe kile.
 
Inaums sana
Waibe hela wengine,sisi tulipe deni? Hii haikubaliki. Tibaijuka na wenzako mkalipe deni
haha mkuu unaota huku unatembea! Kwahiyo mlima klm utauzwa ili sis walipa kodi tusito hizo fedha? Hebu nieleweshe serekal itatoa wap hela?
 
Tanesco wanadaiwa pesa kwa kuvunja mkataba na iptl
 
nani awawajibishe sasa wanavojua kulindana, ingekuwa kwengine wangekua washataifishwa mali adi kizazi cha mwisho fasta tu,na death penalty juu!
 
ESCROW INAENDELEA KULITAFUNA TAIFA

Kwanini Rais Magufuli hafanyii Kazi suala la IPTL? Matapeli hawa wataendelea kuipa hasara Nchi yetu mpaka lini? Sasa mahakama ya ICSID imeamua kuwa Benki ya Standard Chartered ilipwe Shilingi Bilioni 300 na riba. Kiwango Hicho Ni zaidi ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda.

TANESCO wanaingia Hasara hii Kwa sababu ya wizi wa Fedha za TEGETA Escrow na Rais bado anavuta miguu kuchukua hatua dhidi ya suala hili. Nini kimemkuta Rais Magufuli? Rais Kwani...ni hashughulikii Ufisadi huu wa IPTL/PAP? Nini Kinamzuia Rais Kuchukua Hatua dhidi ya Wizi huu wa Dhahiri Kwa Taifa

Tanzania Tunapata Hasara mno, Na Hizi zote Ni Fedha za Wananchi zitakazopotea.

• Watanzania mmelipa matapeli Fedha zilizokuwa kwenye "TEGETA escrow account", Fedha ambazo ziligaiwa Kwa Viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri.

• Watanzania Mmewapa Mtambo wa kuzalisha umeme matapeli hao na mnaendelea kuwalipa "capacity charges" mpaka sasa - Kinyume Kabisa na Maazimio ya Bunge yanayotaka Mitambo Husika itaifishwe.

• Baada ya Hukumu hii Watanzania tutawalipa Standard Chartered Fedha zao kwa mtambo ambao sio wenu na Kwa Fedha ambazo (Kama tungelazimika Kulipa) tungezitoa kwenye Akaunti ya Escrow - Lakini sasa tutazitoa Hazina zikiwa ni Kodi za Watanzania.

Ushauri Wangu - Rais achukue Hatua Zifuatazo

• Awafikishe Mahakamani watu wote waliohusika na kuitia Nchi hasara katika sakata la TEGETA Escrow.

• Aitwae mitambo ya IPTL kisheria na kuimilikisha Kwa TANESCO (Kama ilivyoazimiwa Na Bunge).

• Amkamate Bwana Harbinder Singh Seth na wafuasi wake wote na kuwafikisha Mahakamani Kwa makosa ya Utapeli, Wizi, Uhujumu Uchumi, Utakatishaji wa Fedha nk.

• Ahakikishe Taifa halilipi Fedha Hizi Kwa Standard Chartered. Benki iliyotumika Kupitisha Fedha za TEGETA escrow ndio ilipe Hilo deni tunalotakiwa kulipa.

MUHIMU: Rais AAMUE Kusimama na WATANZANIA au kusimama na "Matapeli wa TEGETA escrow".

Zitto Kabwe Ruyagwa
 
KUNA VITU SIVIELEWI ELEWI HAPA!!!!!!, SASA NITAONA KWA MACHO YANGU UMAKINI WA RAISI WETU, KWANZA HUYO WAZIRI WAKE ALIPOTOSHA TAIFA KUPITIA BUNGE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…