Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

so unawaamini sana hao wazungu na mahakama yao fake?,
hao ni international conmen ,mkiwalegezea mtauza hadi nguo za ndani kuwalipa,na ikishaa hiyo utasikia kumbe standard chartered hongkong nao waliuza deni kwa swiss bank ambao nao wamefungua kesi ya madai dhidi ya Tanesco,mtakamuliwa mpaka basi..
Ilimu ilimu ilimu
Kwa nini tuliwapelekea hao wazungu kesi kama tunawaamini ni feki?
 
Pesa za kempeni tungetoa wapi jamanii???Lakini msihofu tumeambia hakuna mwananchi atakayefatwa kwake kulipa deni.Kidumu chama chetu.
 
Jamani huyu singasinga bado yupo mitaani? tukamateni huyu na mwenzie rugemalila sasa hivi kabla hajasepa, muda unakwenda, takururu +polisi mko wapi?. Huyo muhindi inatakiwa leo alale ndani, yaani huyu singasinga ni wa kunyonga , hakuna haja ya kesi, tunatakiwa tukimkamta hapo ahukumiwe. Hii nchi ni bora hata Somalia kwa kweli, kwani haiwezekani tukaliuza hili nchi halafu kila raia akapewa chake aende akatafute kokote duniani mahali pa kujificha? yaani bunge limezuia malipo kwa PAP wao wakafanya ujanjaujanja hayo yote ili wapige tu, hivi bil 300+ hivi ni viwanda vingapi? hizi ni ndege ngapi ambazo tunaweza nunua kufufua ATCL? hapa hakuna maendeleo kwa mchezo huu.
 
Waibe hela wengine,sisi tulipe deni? Hii haikubaliki. Tibaijuka na wenzako mkalipe deni
Kumbuka Tibaijuka alipewa pesa toka kwa mbia wa IPTL ambaye alistuka kwamba pesa za IPTL na Tanesco zinapigwa! Kwa hiyo pesa yetu haikuchukuliwa na hawa tunao wafahamu bali majizi yaliyo lipwa kupitia Stanbic bank ambayo wamegoma kuwataja!
 
Duh!!! Kwahiyo mwanasheria aliyejiuzuru kwenye sakata hili alikuwa sahihi.
 
Nchi yetu watu wanasoma kama wanakalili mistari ya diamond ndo matokeo yake wakikutana na vichwa vilivyoingia chimbo kwenye mikataba na kwenye kesi lugha yenyewe ni utata kama hatujaondoa mwendo kasi tutaisoma tu
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Hiki ndicho kinapelekea watanzania kuendelea kusoteshwa mazima. Kwa mawazo na akili yako unafikiri shirika linashindwa kufanya kazi ama wafanyakazi au viongozi ni dhaifu? Hujajua tu tatizo liko wapi pamoja na mambo yote yalivyo wazi nyakati hizi! Serikali isipoamua kuweka sawa maswala yote yanayohusiana na umeme na mikataba yake unafikiri kuna dawa?
Hivi we kizibo umenielewa nilichokimaanisha ama unachangia ukiwa tumbo wazi?
 
Kumbuka Tibaijuka alipewa pesa toka kwa mbia wa IPTL ambaye alistuka kwamba pesa za IPTL na Tanesco zinapigwa! Kwa hiyo pesa yetu haikuchukuliwa na hawa tunao wafahamu bali majizi yaliyo lipwa kupitia Stanbic bank ambayo wamegoma kuwataja!
Mkuu kumbe kuna ambao walikula mgao wa TEGETA ESCROW na hawakutajwa?
 
Shamba la bibi,huku walishajipigia huko nao zamu yao halinaga mwenyewe
 
Naombeni mnijuze je kuna uhusiano wa moja kwa moja wa zile hela walizolipwa akina Setti Singh na Rugemalira ambazo kikwete alituaminisha sio za serikali? Najua alielewa kilichofanyika ndio maana alisema vile! kama kuna uhusiano ni wakati wa KUNYONGA watu naaapa!
 
Mnatamani sana Serikali ipandishe bei ya umeme ili muwe na ajenda majukwaani. Mmeula wa chuya. Hilo halitarokea kwa utawala wa Rais Magufuli
Mkuu Lizabon,mada iliyopo mezani ni hilo deni ambalo ni pigo kubw kwa Taifa. Yaani mada yote hiyo ndiyo uchangie maneno machache tena yakikosa kabisa hoja.
Tuache ushabiki wa kitoto kwenye mambo ya maana.
 
Magufuli itabid akomae nalo hili swala kwa manufaa ya watanzania
 
Wote waliohusika na wizi wa pesa za escrow na waliopokea rushwa ya pesa zile wakamatwe mara moja na warudishe pesa zote na wafilisiwe mali zao mara moja.
 
Tanzani ya viwanda namwonea huruma Rais wangu Magufuli maana hii nchi alivyoikuta inabidi ajitoe ufahamu kuiongoza watu wenyewe kuelewa ni shida yaani yahitajika Maombi kwa kweli Mungu aingilie kati.

Ameikuta? Yuko serikalini kwa miaka 20. Kawa waziri na naibu waziri kwa kipindi chote icho.
 
Back
Top Bottom