Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

1.jpg

Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imegeuziwa kibao katika suala la Escrow, imefahamika.

Kampuni hiyo imetakiwa kurejesha zaidi ya Dola za Marekani milioni 100 (Sh bilioni 216.2 ) kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zikiwa fedha za ziada ambazo ililipwa kabla ya hesabu kufanywa upya.

Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Biashara uliotolewa Septemba 12 mwaka huu unaoitaka Tanesco kuilipa Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) Dola za Marekani milioni 148.

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo kutokana na kesi iliyofunguliwa na Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) dhidi ya Tanesco ikidai kulipwa Dola za Marekani milioni 369.
Kwa mujibu wa Wakili wa Tanesco, Richard Rweyongeza, amesema walichokuwa wanabishania mahakamani si Tanesco kulipa bali walikuwa wanabishania shirika hilo litalipa kiasi gani na linamlipa nani.

“Kabla hatujaingia katika kutetea kesi hiyo, mwaka 2014 mahakama hiyo ilisema inayo madaraka na ikaamuru Tanesco kuilipa SCB-HK.
“Sisi tuliingia kutetea baada ya uamuzi huo, Mei, 2014 tukaomba hesabu zifanyike upya kwa malekezo yaliyotolewa na mahakama hiyo kujua deni halisi.
“Hesabu zilipofanyika kwa mtaji wa mwekezaji, walichukua mkopo wakahesabu kuwa ni mtaji, hatua hiyo ilikataliwa na mahakama.

“Kabla ya hesabu kufanyika ndipo likaingia suala la akaunti ya Tegeta Escrow. Fedha zilipochukuliwa katika akaunti hiyo, SCB-HK wakabadilika wakasema hakuna haja ya kufanya hesabu upya kwa sababu Tanesco wamekubali viwango hivyo ndiyo sababu waliwalipa IPTL.
“Tulibishania hoja hiyo ya kulipa kwa viwango vya zamani ikaamuriwa hesabu zifanyike upya, mahakama ilikubali hesabu ifanyike kwa kutumia mkopo wa wana hisa.
“Baada ya kuamuru hivyo, deni likashuka kutoka walichokuwa wakidai Dola za Marekani milioni 369 hadi kuamuriwa kulipa Dola za Marekani milioni 148,”
anasema Wakili Rweyongeza.
Alisema IPTL walilipwa Dola za Marekani milioni 246 kwa kutumia viwango vya zamani na kwamba uamuzi uliotolewa unaanza kutumika katika kipindi chote ambacho Tanesco ilikuwa inadaiwa mpaka mwaka 2015.

“Kutokana na hesabu hizo gharama ilikuwa chini, IPTL ililipwa zaidi hivyo inatakiwa kurejesha Dola za Marekani zaidi ya milioni 100 kwa Tanesco,”alisema.

Rweyongeza alisema walipendekeza SCB-HK wadai fedha zao kwa IPTL lakini mahakama hiyo ilikataa na kuamuru Tanesco ndiyo walipe hivyo kwa mtazamo wa kawaida IPTL inatakiwa kurejesha fedha kwa shirika hilo.

Katika kuhitimisha, mahakama hiyo ilisema pande zote mbili zinazopingana zilishinda katika maeneo muhimu waliyokuwa wakibishania lakini zilipoteza katika hoja nyingine.
Baada ya kumaliza kusikiliza kesi hiyo mahakama iliamuru pande hizo mbili kulipa gharama za usuluhishi na nyingine kwa viwango sawa.

Malipo hayo na anayelipwa katika mabano ni Dola za Marekani 254,775.02 (Profesa MC Rae), Dola 171,278.36 (Profesa Douglas) na Dola 370,126.76 kwa ajili ya Profesa Stem.
Gharama nyingine zilizokadiriwa moja kwa moja ni Dola za Marekani 157,336.26 na gharama za utawala kwa mahakama hiyo Dola za Marekani 180,000 ambako jumla ya gharama zote wanazotakiwa kulipa Tanesco na SCB-HK ni Dola za Marekani 1,133,516.42.

Hata hivyo Rweyongeza alisema pamoja na ushindi huo hawakuridhishwa na uamuzi huo kwa sababu katika uamuzi wa kwanza, mahakama hiyo ilikataa hesabu kupigwa kwa kutumia kiwango cha 22.31 lakini bado katika uamuzi huu walitumia kiwango hicho kufanya hesabu hivyo walikosea kufanya hivyo.

Hoja ya pili, alisema SCB-HK si mwekezaji hivyo hakustahili kupeleka kesi hiyo mahakamani na kwamba hapakuwa na hoja.
“Sababu nyingine ya kutoridhishwa na uamuzi huo ni kwamba hatukupewa nafasi ya kujibu hoja mpya zilizowasilishwa kuhusu Tanesco kwamba ilidanganya, tulipaswa kujibu kwa maelezo ya mashahidi si mawakili.
“Tuliwasilisha hoja kwa maandishi, zilipotokea hoja mpya tulitakiwa kuzijibu kwa kuleta mashahidi, tunapinga pia uamuzi ulioitambua SCB-HK kuwa ilistahili kisheria,”
alisena Rweyongeza.
Suala hilo limeibuka ikiwa imepita miaka mitatu tangu Serikali kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini kuruhusu kufanyika kwa malipo ya Dola za Marekani milioni 200 (zaidi ya Sh bilioni 300) kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Fedha hizo zilitolewa na kwenda kwa mmiliki wa Kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP), Harbindar Singh Sethi mwenye makazi yake nchini na Afrika Kusini.
Katika kesi hiyo Tanesco ilikuwa inawakilishwa na mawakili wa kampuni za R.K Rweyongeza & Advocates na Crax Law Partners.

Chanzo cha Escrow
Mwanzoni mwa miaka ya 1990 nchi ilikuwa na upungufu wa umeme kutokana na upungufu wa maji kwenye mabwawa, ambapo 1994 serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa IPTL ilikuwa iliyokuwa ikimilikiwa na VIP ya Tanzania iliyokuwa na asilimia 30 na Mechmar ya Malaysia yenye asilimia 70.
Tanesco na IPTL walisainiana mkataba wa miaka 20, hata hivyo uzalishaji haukuanza mara moja kutokana na mgogoro ulioibuka baina yao (Tanesco na IPTL) .

Mwaka 2002 IPTL ilianza kuzalisha umeme na mkataba ukaanza kuhesabiwa hapo, lakini kutokana na mgogoro ikafunguliwa akaunti ya Escrow na mwaka 2004 Tanesco ilifungua shauri kupinga tozo la Capacity Charge

Uwiano wa mtaji ni 70 kwa 30 na uamuzi haujabadilishwa na mahakama yoyote. Mwaka 2004 Kampuni ya Mkono & CO advocates iliishauri Tanesco iendelee kupinga Capacity Charge London.
Inaelezwa kuwa Agosti 2005, benki ya SCB-HK ilinunua kwa bei ya punguzo ya dola za Marekani 76.1 kutoka Benki ya Malaysia ya Danaharta baada ya kushindwa kurejesha deni la muda mrefu kutoka IPTL.

Bei halisi ya deni hilo ilikuwa ni dola milioni 101.7 kwa mujibu wa ushahidi uliopo ambako IPTL ilikopa dola milioni 100 mwaka 1998 kutoka kwa mbia wa benki ya Malaysia ili kujenga mtambo wa kufua umeme wa megawati 100 wa Tegeta.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, SCB-HK ilipewa kandarasi kadhaa ikiwamo haki ya kulipwa deni la 1997, ambako mkataba wa utekelezaji na hatia ya makubaliano ya dhamana iliyosainiwa kati ya IPTL na Serikali.

Fedha zilivyotolewa
Akaunti ya Tegeta Escrow ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya ufuaji umeme baada ya Tanesco kuingia kwenye mgogoro na Kampuni ya IPTL na suala hilo lilipelekwa mahakamani.

Kwa mujibu wa masharti ya uendeshaji wa akaunti ya Escrow, fedha zilitakiwa zitolewe baada ya Mahakama kutoa uamuzi wa mgogoro huo, lakini wakati ilitaka pande hizo mbili zikutane na kukokotoa viwango vya tozo, fedha hizo zilitolewa na kulipwa mmiliki wa Kampuni ya Pan Africa Power Solution (PAP) jambo lililosababisha kuibuka kashfa hiyo.

Ilivyotua bungeni
Aliyekuwa wa kwanza kulifikisha bungeni suala hilo ni aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ambaye aliwalipua baadhi ya mawaziri wa Serikali ya awamu ya nne kuhusika na mpango huo.
Hatua hiyo ilisababisha Spika wa Bunge la 10 kuagiza uchunguzi wa vyombo vya dola kuweza kuchimbua kwa undani wizi huo.

Baada ya kukamilika ilikabidhiwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAP) chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake Zitto Kabwe na Makamu wake, marehemu Deo Filikunjombe.

Novemba 28 mwaka 2014, Bunge la 10 lilitoa maazimio manane kuhusu suala hilo huku Harbinder Singh Sethi, James Rugemalira wa (VIP), aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme wa Umeme Tanzania (TANESCO) walionekana kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha kufanyika miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta kwenda Pan African Power Solutions Ltd (PAP) na VIP.

Bunge pia liliazimia mawaziri wa wakati huo wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wa kati huo, Eliachim Maswi na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO wawajibishwe kwa kuishauri mamlaka yao ya uteuzi kutengua uteuzi wao.

Mawaziri hao walipoteza nyadhifa zao huku Profesa Muhongo akijiuzulu na Tibaijuka uteuzi wake ukifutwa na Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.


CHANZO: Mpeukzi
Credit: Mtanzania
 
Jk alishasema fedha z escrow sio mali yetu sasa leo iptl walipe nini.
Zile walizogawana ndio wanatakiwa wastakiwe hela zirudishwe
 
TANESCO IMESHINDA
Rweyongeza alikuwa akitoa tafsiri yake ya kisheria juu ya mgogoro huo uliofikia tamati Septemba 12.
====================
Kizungumkuti....!Na mimi nikija na ya kwangu nitaambiwa ni mchochezi?
 
mbona haeleweki....hili ni janga kwa kweli yaani unaambiwa ulipe bilioni zaidi ya 300 zen unasema wewe ndo umeshinda duuu...
 
...mmeshindwa kesi lalfu mnajipongeza!..this is only in TZ... just amazing.....
 
Kwa hiyo hao PAP wana pesa za umma?kwa hiyo kwene escrow kulikuwa na pesa za umma?MESSAGE SENT
 
Ni hivi Harbinder Seth Singh alihakikishia serikali hawezitokea third party kudai ile pesa ya ESCROW sasa hapa inakuwa je hukumu ilishatoka na tumeshindwa? Seth rudisha pesa.
 
Ambacho hujakizungumzia ni jurisdiction. Je hiyo mahakamani iliyoamua mmiliki ni PAP ilikuwa ina uwezo huo, na sheria iliyotumika ni sahihi? Kama Tanesco walingia mikataba kutumia English law, huwezi tu kujiamulia kutumia sheria na mahakama za Tanzania. Soma kwanza hukumu nzima.
Soma bandiko lenye maelezo ya TANESCO ndio kile kile nilichokuwa nawaeleza. Kosa la TANESCO ilikuwa kukubali kusikiliza upuuzi wa wazungu ilitakiwa wawaelekeze IPTL ndio waliokopa huko kabla ya kuanza ku deal nao directly.
 
Kosa la TANESCO ilikuwa kukubali
Kama ni kosa, kwahiyo wamekosea hivyo watalipishwa hiyo faini, au? Ndio maana nikasema "Tanesco" katika hii kesi walikuwa wanajua wanafanya nini, na gharama au matokeo yake yatakuwaje. Manake maamuzi ya mahakama ya Benki ya Dunia yako wazi kabisa, aliyeshindwa ni nani.
 
Tuamue wenyewe: Tanzania ya XX ni ya viwanda.. inawekana?? viwanda hivyo vitatumia nishati gani??? shirika ambalo linatakiwa kuongeza uzalishaji wa umeme, sasa linadaiwa mabilioni ya fedha, wafadhili nao wamegoma kutoa fedha za REA, je hivyo viwanda tutavijenga na kuviendesha kwa kutumia nishati gani?
 
Soma kwanza hizi extracts from post [HASHTAG]#562[/HASHTAG]

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo kutokana na kesi iliyofunguliwa na Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) dhidi ya Tanesco ikidai kulipwa Dola za Marekani milioni 369.

Kwa mujibu wa Wakili wa Tanesco, Richard Rweyongeza, amesema walichokuwa wanabishania mahakamani si Tanesco kulipa bali walikuwa wanabishania shirika hilo litalipa kiasi gani na linamlipa nani.

Rweyongeza alisema walipendekeza SCB-HK wadai fedha zao kwa IPTL lakini mahakama hiyo ilikataa na kuamuru Tanesco ndiyo walipe hivyo kwa mtazamo wa kawaida IPTL inatakiwa kurejesha fedha kwa shirika hilo.

Hoja ya pili, alisema SCB-HK si mwekezaji hivyo hakustahili kupeleka kesi hiyo mahakamani na kwamba hapakuwa na hoja.
“Sababu nyingine ya kutoridhishwa na uamuzi huo ni kwamba hatukupewa nafasi ya kujibu hoja mpya zilizowasilishwa kuhusu Tanesco kwamba ilidanganya, tulipaswa kujibu kwa maelezo ya mashahidi si mawakili.
“Tuliwasilisha hoja kwa maandishi, zilipotokea hoja mpya tulitakiwa kuzijibu kwa kuleta mashahidi, tunapinga pia uamuzi ulioitambua SCB-HK kuwa ilistahili kisheria,”
alisena Rweyongeza.

...................................................................................................................................................................................

Mkataba unakuwa na kitu kinaitwa offer, offeror and offeree; hakuna mahala TANESCO na HSC-Bank wanaizo connection directly. Hivyo ndio vigezo vinavyobainisha involved parties in any contract dispute.

Mikataba halali iliyopo ni TANESCO na IPTL
Nyingine ni IPTL na Malaysian Bank (iliyofilisika) na deni lao kununuliwa HSC-Bank

Sasa wao badala ya kuwaelekeza hao watu waanzie wapi wakajiingiza mkenge wa kuanza ku deal nao directly na kufanya mambo mengine ya kipuuzi; huko walipoenda kufungua kesi ya mgogoro wa capacity charge badala ya kuwaita IPTL wakaanza ku deal na wazungu pia. Ni kuwapa nafasi ya kisheria kutambulika kama wanadeal na TANESCO directly.

Na ndio unaona ata maelezo ya mwanasheria wao kama vile ajielewi anaongea hiki anakataa kile kwenye hizo abstract nilizokuwekea. Mambo mengine in details kuweza kuyaelezea kwa kina inataka kuona mikataba yote kwa kina na kusoma terms zake.

Hila kwa kuwa TANESCO washalipa hizo hela, na walitaka mahakama itambue PAP akija mdeni mwingine azirudishe ina maana kisheria PAP ataamuliwa azirudishe hizo hela au afungue na yeye kesi nyingine ya kupinga maamuzi ya makahama ya ICSD on the basis ya kuwa SCB hana mkataba na TANESCO bali yeye. Lakini TANESCO alishajikinga na hela za escrow account.
 
Back
Top Bottom