SoC02 TEHAMA inabeba ajira

SoC02 TEHAMA inabeba ajira

Stories of Change - 2022 Competition

craade

New Member
Joined
Aug 12, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Najua utakuwa umeingia na kusoma nakala hii sababu ya kichwa cha hii nakala, lakini ukweli ni kuwa ingawa tehama ina leta maendeleo lakini pia katika upana wake inasababisha upotevu wa ajira kwa wananchi, tunajua mashine na mifumo imekuja kurahisisha ufanyaji kazi wa mambo mengi na pia kubadili mfumo wa maisha.

Zamani ilikuwa unaweza kuuza zaidi ikiwa duka lako liko eneo zuri lenye mzunguko mkubwa wa watu lakini siku hizi kuna mitandao ya kijamii pamoja na tovuti za biashara(e-commerce websites) ambapo wewe unaweza ukawa unauza zaidi ukiwa nyumbani na huna duka kuliko hata yule ambaye duka lake liko sokoni ama kituo cha mabasi.

Ukienda kwenye kilimo zamani tulikuwa tunaajiri wamama na wababa shambani kusaidia kupanda na kuweka matuta lakini siku hizi vyote vinafanyika kwa kutumia viambatanishi (attachment) za matrekta.

Tehama hakuna wa kuizuia ni muda wake wa kuja na kubadili mfumo wetu wa ajira na maisha kwa ujumla. SASA TUFANYAJE; Swala ambalo ningependa kushauri jamii kwa ujumla ni kuweza badili mtazamo wao pamoja na kuwaasa walimu na mitaala ya elimu ijikite katika ubunifu ili kuweza kwamua jamii kutoka na hili janga la kutokuwa na ajira na kutegemea ajira.

Tunapo elekea hatuta hitaji matrafiki wengi, wadada wa kazi, deiwaka, wauza magazeti, makonda, dereva boda maana tumeona katika nchi zilizo endelea kuna scooters, mashine za deki na kufua, magazeti ya kimtandao, mataa yanaongozwa na mfumo (remote traffic lights controlling systems).

TUBADILI MITAZAMO CHANGAMOTO NI FURSA AMKA...
 
Upvote 2
Back
Top Bottom