Huenda dunia ya muziki ikampoteza kabisa rapper 6ix9ine, Imeripotiwa kuwa baada ya kutoa ushahidi Mahakamani dhidi ya kundi lake la "Nine Trey Gang" ataingia kwenye utaratibu maalumu wa kulindwa na serikali baada ya kutoa ushahidi (Witness protection) kwa kuhofia maisha yake.
.
6ix9ine akiwa chini ya utaratibu huo atalazimika kubadilisha kila kitu kwenye maisha yake ikiwemo kazi, jina, mahali pa kuishi na vitu vingine, Pia atalazimika kubadilisha muonekano wake ikiwemo kuzitoa nywele zake maarufu za rangirangi na kufuta tattoo za usoni na vyote vitaghramikiwa na waendesha mashtaka.
.
Kabla ya kukubali kushirikiana na waendesha mashtaka #6ix9ine alikuwa anatazamia kifungo cha miaka hadi 49.
CREDIT: Wasafifm