Teknologia ya kisasa ya kuzima moto "ELIDE FIRE BALL EXTINGUISHER"

Teknologia ya kisasa ya kuzima moto "ELIDE FIRE BALL EXTINGUISHER"

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
6,076
Reaction score
15,685
ELIDE FIRE EXTINGUISHER ni teknologia ya kisasa ya kuzima moto bila kuleta athari yoyote kwenye mazingira na watu.

HISTORIA YA ELIDE FIRE EXTINGUISHER
Hii teknologia iligunduliwa mwaka 1997 na raia Thailand aliyeitwa Phanawatnan Kaimart katika mji wa BANGKOK, Thailand.

Baada ya kunusurika kifo katika ajali ya moto iliyotokea katika Hotel ya Royal Jomtien Resort Hotel iliyopo mji wa Pattaya mwaka 1997 ambapo inakadiriwa watu wiapatao 100 walipoteza maisha.

Alivumbua huu mpira wa kuzima moto baada ya kuona maafa ya moto na idadio kubwa ya watu waliopoteza maisha baada ya mitungi na njia za kuzima moto za kawaida kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

JINSI KIFAA HIKI KINAVYOFANYA KAZI
Moto ili utokee lazima kuwe na vitu vitatu 1.Kitu cha kuungua (Fuel) 2. Hewa ya oksijeni (Oxygen) 3. Joto (Heat).

Elide Ball itafanya kazi endapo itatokea moto na itaji activate yenyewe ndani ya sekunde 3 mpaka 10 baada ya kuhisi joto au mtumiaji kuisukuma kwenye moto.Kwenye huu mpira ndani kuna fuse ambayo hufunguka baada ya huu mpira kufika katika moto na lile kava la nje huondoa oksijen iliyopo na powder yenyewe hufanya kazi ya kuzima moto.

Hii imetengenezwa kwa Mono Ammonium Phosphate Chemical Powder ambayo ipo ndani ya huu mpira inaenda kufanya kazi ya kuzuia vichochezi vitatu vya moto kutofanya kazi.

FAIDA ZA HIKI KIFAA
1. Hakihitaji elimu ya uzimaji moto mtu wa rika yoyote anaweza tumia.
2.Rahisi kubebeka kina uzito wa kilo 1.5 na kipenyo cha duara cha 152cm.
3.Unaweza ukaweka sehemu zile zenye uwezekano mkubwa wa moto kutokea
4.Kina alarm ya onyo ambayo inasikika mpaka umbali wa mita 200
5.Kinafanya kazi ndani ya muda mfupi sekunde 3 mpaka 10.
6. Hakihitaji gharama za marekebisho, life span yake ni miaka 5.
7. Kinatoka na stendi yake ya chuma kwa ajili ya kuifadhia
8. Baada ya kuzima moto hakileti uchafuzi wa mazingira na kumdhuru mtumiaji.
9.Hakitoi alarm za uongo kama fire detector, hiki hutoa alarm endapo kuna moto na kuuzima.
10. Sauti ya alarm ni 120-140dBA ambayo haina madhara kwa binadamu.

AINA ZA MOTO UZIMWAO NA ELIDE FIRE
1.Moto daraja A- Moto utokanao na mbao,karatasi na fabric.
2.Moto daraja B- Moto utakanao na vimiminika viwakavyo (Flamable liquids) Petrol,Diseli na Mafuta ya taa.
3.Moto daraja C- Moto utokanao na gesi (Flammable gas) kama gesi za majumbani LPG. Gesi kama CNG,LPG na nyinginezo.

Elide Ball Fire extinguisher imetestiwa zaidi ya mara 50,000 na mataifa ya Ulaya,Marekani na Asia wamekipitisha na kimeshinda tuzo za ubora wa kimataifa.

PENDEKEZO
Serikali kupitia jeshi la zimamoto na uokoaji, watu wa usalama mahala pa kazi inabidi washauri watu wenye viwanda, magari, hotel na sehemu zenye mikusanyiko ya watu au hatari ya kutokea moto kifaa hiki kitumike kama njia ya kuzima moto na kujihami.

Baadhi ya nchi za ulaya kwenye gari ndogo hiki kifaa kinawekwa mbele ndani ya boneti, endapo moto ukitokea ghafla unazimwa na hiki kifaa haraka.

Fire_Ball_Info_2_.jpg
 
So, hakifai kutumika kuuzima ule moto unaoteketeza msitu wa mapafu ya dunia kule Brazil?
 
Back
Top Bottom