Kwa Dunia ya sasa, vijana ndio binadamu walio kwenye hatari kubwa ya kupotea kuliko wazee. Kutokana na ukuaji wa teknolojia, vijana wengi wamejikita kwenye kuigiza maisha mtandaoni huku hali halisi ikionesha maisha magumu na wengi wao kutojua suluhisho ni nini. Mfano, mitandao mingi ya kijamii kama Facebook, Instagram, TikTok na Twitter imechangia sana katika ukuaji wa msongo wa mawazo huku wengi wakilinganisha maisha yao na wahusika wengine wanaotumia mitandao hiyo ambao wanaonekana na maisha mazuri hasa katika umri mdogo.
Tamaa ya Mali na kufanikiwa, hupelekea vijana wengi kuishia kujilaumu na kuona maisha kwao hayajawa sawa. Ni jambo la kisaikolojia linalosumbua idadi kubwa ya watu hasa vijana wanaotumia muda wao mwingi katika matumizi ya vifaa vya mawasiliano vya kielektroniki kama simu janja, vishikwambi na kompyuta mpakato kuperuzi taarifa mbalimbali , kutumiana jumbe fupi na hata kutumika katika biashara za mitandaoni.
Ni jambo Lisiloongelewa sana Kwa nchi nyingii za Afrika, lakini msongo wa mawazo ni Hali inayosambaa Kwa Kasi ikichochewa na ukuaji wa sayansi na hasa teknolojia. Watu wengi hasa rika ya vijana ni wahanga wakubwa wa hii hali na jamii Kwa ujumla haitilii maanani uwepo wa hili tatizo hivyo kupeleka usambaaji na ukuaji wa waathirika.
Kwa akili ya binadamu wa kawaida, njia rahisi ya kupunguza msongo wa mawazo ni mawasiliano yaani kuongea jambo linalosababisha mtu apate mawazo na hivyo kutafuta suluhisho la tatizo husika. Lakini Kwa sasa watu wengi wenye msongo wa mawazo wamekimbilia kwenye unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na kushiriki kwenye mambo maovu Kwa kutegemea kupata amani ya moyo na akili na hivyo kuepukana na maumivu wanayopata wanapokuwa na msongo wa mawazo.
Lakini matumizi ya vilevi ndio yanayomuongezea mhusika maradhi ya mwilini kama ugonjwa wa moyo, mapafu na ini hivyo kupeleka matatizo kuongezeka badala ya kupungua kama inavyotegemewa.
Jamii imepunguza ukaribu na watoto pia vijana, huku Kila mtu akijikita kwenye matumizi mengi ya muda kwenye kutumia vyombo vya kielektroniki kama kompyuta mpakato, televisheni na simu bila kujali muda wa familia kukaa pamoja au ni muda wa marafiki kujuliana hali.
Matumizi makubwa yasiyo ya lazima ya vifaa vya kielektroniki yanasababisha upweke Kwa watoto wanaoelekea ujana, ambao wanajikuta wanakosa muda na mwongozo wanaotegemea kuupata kutoka Kwa watu wazima katika familia au jamii na hivyo kupeleka migawanyiko katika familia nyingi.
Msongo wa mawazo ni jambo lisilofichika na lipo katika jamii zetu lakini uoga wa kujieleza unapeleka watu wengi kuathirika bila kupata msaada.
Tumeona idadi kubwa ya vijana wakijihusisha katika matukio ya ulevi wa kupindukia, mauaji/kujiua na matumizi ya bangi,mara nyingi jamii ikihoji mienendo mibaya ya tabia za wahusika lakini tukisahau kutazama upande mwingine wa wahusika na kujiuliza je, muhusika alikuwa akisumbuliwa na matatizo gani au kupata mda wa kuhoji chanzo kikuu Cha kuchukua maamuzi wanayoamua kuchukua.
Kushindwa kuwaza hivo kumechangiwa na upungufu wa mawasiliano baina ya wanafamilia, marafiki na wanajamii.
Kwa ukubwa na upana wa Hali ya msongo wa mawazo, ni muhimu Jamii ikajikita kwenye utatuzi wa hili tatizo la sivyo ni rahisi uongezekaji wa matukio ya kiuhalifu ambayo yanaumiza mtu mmoja mmoja na taifa Kwa ujumla.
Msongo wa mawazo ni Hali inayomtafuna mtu angalia hai, na kufanya kupoteza Kwa utu wa mhusika mwenyewe kama binadamu wa kawaida. Ni vyema jamii ikihusisha familia, jumuia, marafiki na vikundi mbalimbali kukuza mawasiliano baina yao na watoto wanaoendelea kujua Ili kuepusha uwepo wa msongo wa mawazo ambao vijana wengi Kwa kipindi hiki wanapitia.
Ni muhimu serikali ikaingilia Kati Kwa kuwezesha upatikanaji wa wataalamu wanaohusika na afya ya akili wakiwa tayari kutoa ushauri, matibabu na pia kusikiliza wahitaji Kwa uaminifu.
Hii inaweza kupungza ukuaji wa msongo wa mawazo Kwa kijana mmoja na baadae Kwa asilimia kubwa ya vijana na hawa watu wazima walio na uhitaji.
Familia zinatakiwa ziwajibike Kwa watoto wao, wazazi watumie muda wao kuwasiliana na watoto juu ya maisha ya shule, maisha ya nyumbani na hasa changamoto wanazopitia wapo maeneo yoyote aidha ni nyumbani au sehemu nyingine yoyote. Kujenga uwezo wa kujieleza Kwa mtoto husaidia mzazi kupata taarifa muhimu zinazomhusu mtoto ambazo hataweza kupata sehemu nyingine yoyote.
Mfano matukio ya ubakaji na ulawiti wa watoto yanayozidi pamba moto nchini, wazazi/walezi wanakuwa watu wa mwisho kujua mambo wanayofanyiwa watoto wao, shida ni kutojijenga uaminifu Kwa watoto wao na kukuza roho ya uoga na kutojieleza.
Ni muhimu kutojenga uoga Kwa watoto wanaojua ukiwa wengi wao wakishindwa kueleza hali wanazopitia kutokana na kukua katika mazingira ya uoga.
Taasisi za kidini pia Zina uwezo mkubwa wa kupunguza na kuzuia usambaaji wa tatizo la msongo wa mawazo Kwa vijana na watu wazima.
Viongozi wa dini ni watu wanaoaminika sana na watu na kutokana na mawaidha ya kidini waliyonayo ni rahisi kuepusha jamii na hili tatizo la msongo wa mawazo Kwa kuyatoa mawaidha/mahubiri hayo Kwa waumini wake na hivyo kusababisha amani ya moyo na akili Kwa watu.
Kwa maendeleo ya taifa, ni muhimu nguvukazi iwe vizuri kimwili na hasa kiakili, afya nzima ya mtu ni muhimu kwaajili ya kufanikisha mipango ya mtu mmoja, familia, na taifa Kwa ujumla.
Wakati nchi inahangaikia afya ya mwili ni muhimu afya ya akili itiliwe maanani pia.

Upvote
0