Neema ya BWANA
Member
- Jun 25, 2023
- 45
- 32
Miongoni mwa changamoto zinazolikabili Taifa la Tanzania na Bara la Afrika lakini pia Dunia nzima ni Ajali za Barabarani pamoja na Foleni za Barabarani.
Ajali za Barabarani husababisha aidha kupoteza roho za watu au kuharibu miili na akili za watu jambo ambalo halitakiwi kunyamaziwa hata kwa sekunde moja; huku Foleni za Barabarani husababisha kupoteza muda na kuchelewesha shughuli mbalimbali za kila siku za Ujenzi wa Taifa la Tanzania, Bara la Afrika na Dunia nzima.
Zipo teknolojia mbalimbali za ujenzi wa barabara ambapo kwa sasa ndizo zinazotumika; na barabara hizi si nyingine bali ni Barabara za Lami. Barabara za Lami zipo za aina, mitindo na miundo tofauti tofauti lakini pamoja na hayo yote bado barabara hizi zimeelemewa na changamoto za ajali na foleni.
Swali ni je! Tatizo ni nini?
Tatizo kubwa la ajali za barabarani na foleni za barabarani ni mfumo mzima wa Ki-Teknolojia katika huduma ya usafirishaji; yaani mfumo wa barabara zenyewe na mfumo wa vyombo vya usafiri vinavyotumika. Tutawalaumu Madereva Bure! Tutawalaumu Watu wa Usalama Bure! Tutazilaumu Serikali Bure! Lakini tujiulize swali moja, je! Mfumo wa Teknolojia ya Usafiri tuliyonayo iko sawa na haina dosari yoyote?
Hapa kila mtu atakuwa na majibu yake, lakini UKWELI ni kwamba Mfumo wa Teknolojia ya Usafiri tulio nao sasa Nchini Tanzania, Barani Afrika na Duniani kwa ujumla uko 'very complicated' kiasi kwamba hata tunaposafiri kwenda maeneo mbalimbali tunapofika salama tunakokwenda ni MUNGU TU MWENYEWE Ndiye Anayetufikisha salama, kwani bila YEYE hakuna ambaye angeweza kuepuka 'ugumu' uliopo kwenye Mifumo yetu ya kusafiria.
Ni kweli ajali mpaka itokee ni suala la kiroho na kimwili, lakini kwa HEKIMA YA MUNGU tunao UWEZO wa kutompa nafasi shetani nafasi ya kusababisha ajali hizi.
Hebu fikiria;
Gari la kawaida lina uzito wa tani kati ya 1 mpaka 1½, huku magari makubwa yakiwa na makumi kadhaa ya tani, ambapo gari hilohilo hupandisha watu na mizigo ambayo hupelekea uzito uendelee kusoma; lakini gari hilihili ndilo linaendeshwa na dereva mwenye uzito wa Kg 50-80 kwa urefu wa safari kuanzia Kilomita moja mpaka maelfu ya Kilomita, huku matairi ya gari yakiwa hayazidi uzito wa Kilogram 100 mpaka Kilogram 500.
Gari hili pia ndilo ambalo halifanyi kazi mpaka liwekwe mafuta, lakini mafuta hayohayo ikitokea tatizo kidogo hugeuka kuwa moto na kuteketeza gari; kitendo kinachopelekea kuhatarisha maisha ya walio ndani ya gari.
Kumbuka pia gari hili ndilo lenye kasi ndogo, kasi ya kati na kasi ya juu kabisa hivyo maamuzi yanabaki kuwa ya dereva, atakavyoamua ndivyo mtakavyoendeshwa.
Gari hili ndilo ambalo mvua yaani mvua ambayo si ya vitone bali mvua ambayo husababisha maji kutiririka juu ya kioo; ikiwa inanyesha hata dereva akisafisha kioo hakiwezi kuwa clear kabisa badala yake itawapasa madereva kuwasha taa hata kama ni asubuhi au mchana; japo pamoja na taa hizo kuwashwa kuonana gari kwa gari huwa ni kwa mbali sana.
Gari hili ndilo ambalo matairi yake huweza kuchomoka muda wowote hususan dereva akiamua kuchagua mwendo wa kasi ya juu.
Gari hili ndilo ambalo pia matairi yake huweza kupata pancha na kupasuka au kupinduka likiwa kwenye mwendo hususan tairi lenyewe likiwa la mbele.
Gari hili ndilo linalotembea maelfu ya kilomita huku madereva wakibadilishana usukani, lakini lenyewe bado linaendelea kwenda mpaka lifike bila kujua kuwa linachoka.
Gari hili ndilo ambalo ndani yake kuanzia siti zake na kila kilichomo muda wowote vinaweza kumgeuka aliye ndani ya gari na kuwa silaha zenye kusababisha kuondoa uhai wake pale inapotokea ajali; kwa mfano yupo mtumishi mmoja wa MUNGU kutoka taifa jirani aliyewahi kufiwa na mkewe ambaye pia alikuwa mtumishi wa MUNGU (mwimbaji wa nyimbo za Injili aliyekuwa maarufu enzi za uhai wake); alipohojiwa kuhusu kifo cha aliyekuwa mke wake alisema ni ajali ya gari ambayo ilipelekea kutobolewa na chuma (au kitu kinachofanana na hicho) maeneo ya kichwani hata kupelekea wigi alilokuwa amevaa kubaki kwenye kitu hicho. Inasikitisha lakini Mapenzi ya MUNGU Ilibidi yatimie.
Lakini pia mbali na hili tukio, yapo matukio mengi mengine ya ajali ambayo vifo vya watu kwenye ajali hizo vilisababishwa na kubanwa na siti ya gari, kuchomwa na vioo vya gari, na kadhalika.
Hiyo ilikuwa ni upande wa magari, lakini pia katika Mfumo wa Barabara hebu fikiria;
Mfumo wa Barabara uliopo duniani ndio ambao mvua ikinyesha barabara zake huteleza.
Mfumo wa Barabara uliopo duniani ndio ambao huelemewa na msongamano pamoja na uzito wa magari huku barabara hizo zikishindana na watu kugombea ardhi pale ambapo idadi ya magari huongezeka hivyo upana wa barabara kutakiwa kuongezeka pia.
Mfumo wa Barabara uliopo duniani ndio ambao pamoja na kuhitaji eneo kubwa la ardhi bado hazitoshi kwani msongamano wa magari na ku 'overtake' bado kunafanyika kwa kiwango kikubwa.
Mfumo wa Barabara uliopo duniani ni sawa na msemo usemao 'wembamba wa reli treni hupita'; bila kujua reli hii hupitia hali gani.
Suluhisho
Ili kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa Ajali za Barabarani Nchini Tanzania, Barani Afrika na Dunia nzima ni bora Mfumo wa Teknolojia ya Usafiri ubadilike kutoka vyombo vya moto vya usafiri na vinavyotembea kisha kuwa VYOMBO BARIDI VYA USAFIRI NA BARABARA ZINAZOTEMBEA.
BARABARA ZINAZOTEMBEA NI NINI?
MFUMO WA TEKNOLOJIA YA BARABARA ZINAZOTEMBEA ni mfano wa 'Conveyor Belt' inayotumika kusafirisha mizigo katika maeneo kama kwenye Viwanja vya Ndege na Viwanda vya bidhaa mbalimbali.
Picha kutoka mtandaoni
Mpigapicha Abu Syed kutoka Dhaka nchini Bangladesh aliwahi kutoa pia wazo kama hili mnamo mwaka 2017 lakini bado haijafahamika mpaka sasa limefikia wapi kwani kuanzisha kitu kipya duniani si rahisi lakini inahitajika NEEMA YA MUNGU PEKEE kwa sababu HAKUNA jambo gumu MBELE ZAKE kikubwa ni kufuata MNYORORO WA THAMANI WA UBUNIFU.
Picha kutoka mtandaoni
Faida ya Barabara Zinazotembea;
Kwanza Barabara hizi huzuia matumizi ya vifaa vya moto ambavyo badala yake juu ya barabara hizi kunatakiwa kuwe na 'Hema' maalum kwa ajili ya kubeba abiria wasafirishwao na barabara hizi.
Kutokana na kutotumika kwa vyombo vya moto, kunazuia uchafuzi wa hali ya hewa ambayo ni moja kati ya changamoto kubwa sana duniani yenye athari za kila aina kwa wanadamu na maisha ya kila siku.
Barabara hizi zinakomesha foleni za magari.
Barabara hizi zinakomesha Ajali za Barabarani kwani mwendo wa usafiri mpaka mpangilio mzima wa usafiri, barabara ndiyo inafanya kwa kuendeshwa na zaidi ya mtu mmoja wenye kufanya kazi moja tofauti na vyombo vya moto viendeshwavyo na watu tofauti kila mtu na tabia yake na anavyotaka yeye.
Uundaji wa mahema unatakiwa kuwa wa KIBUNIFU na unaozingatia matumizi ya SANAA NA TEKNOLOJIA ili mahema haya yawe 'simple but elegant' hata abiria anapoingia na kukaa asitamani kushuka; lakini pia yasiwe na vitu wala viashiria hatari vya aina yoyote vya kuhatarisha maisha na usalama wa abiria.
Barabara hizi hutumia umeme.
Mwisho ni gharama za kujenga barabara hizi; inategemea na 'materials', mtindo na muundo unaotumika, hivyo gharama huweza kuwa za chini, za kati au za juu.

Upvote
2