Telephone business na makosa yanayotugharimu

Telephone business na makosa yanayotugharimu

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Ninapo sema telephone business naongelea biashara ya kuendesha kwa simu, wewe ukiwa unawatumikia watu wengine.


Kuna telephone Farming na telephone businiess.

TELEPHONE BUSINESS.

Hiki ni kitendo cha wewe kuanzisha biashara na baada ya hapo unamkabidhi either.
- Mke/mme
-Shemeji
-Wifi
-Mjomba
-Binamu
-Mama mke/Baba mkwe
-Mama/Baba
Shangazi na kadhalika na pia wafanyakazi.

Ukisha wekeza wewe huwaka bidhi na wewe kuendelea na majukumu ya Kuajiriwa.

Baada ya hapo wewe ni mwenzi wa simu tu.
Hello vipi? Leo mmezuza sh ngapi?
Nini kimepungua?
Wateja vipi leo?

SIKILIZA

Biashara inamuhitaji muanzilishi kuliko mtu yoyote yule nazani naeleweka ninavyo sema mtu yoyote yule angalia hapo juu.

Biashara siku za mwazo za uhai wakw inamuhitaji sana mwenye nayo.

Wewe ndo inititora wa Idea. Kamwe usikaimishe buashara siku za mwanzo.

Biashara ni nama mtoto mchanga ndo maana mzazi hupewa likizo ya miezi 3 ya yeye kunyonyesha.

Miezi mitatu ya mwanzo ni muhimu sana kwa mtoto na mistake pale ndo mtoto anakuwa dhaifu milele.

Wengi wetu huanzisha biashara na kuweka watu wa karibu tukizani ndo suluhisho.

BIASHARA SIO KUDHIBITI MAPATO TU KAMA TUNAVYO AMINISHANA.

TELEPHONE FARMING NAYO.

Hapa ni mwendo wa kulima na kufuga kwa simu.
- Shamba linatafutwa kwa simu.
- Shamba linafyekwa kwa simu.
- Shamba lina limwa kwa simu.
- Linaoteshwa kwa simu.
-Lina paliliwa kwa simu.
Linavunwa kwa simu.

Sitaki kuelezea sana hapa nazani wengi mnajua huwa kuna nini.

Kama unauchungu na pesa na umedhamiria kulima au kufanya biashara ni kuamua moja la sivyo Mshahara wako ndo utakuwa unatumika kuongeza stock ya vitu Dukani au Kuwalipa wafanya kazi.

KWEPA SANA TELEPHONE BUSINESS

Kuna Mdada mmoja alikopa zaidi ya milioni 200 akawekeza kwenye Ufugaji wa Ng'ombe,kuku,Nguruwe, Bata mzinga.

Kwa kifupi ilikuwa ni investment ya kufa mtu yaani nahisi yule Dada angekuwa mbali sana kwa sasa.

Kama kawaida yeye anakuja jioni kunagalia muda mwingin ni simu kwenda mbele.

Ninavyo andika ni kwamba Mkopo hajarudisha na Project isha kuwa historia na Benki wamezuia kila kitu.

Too bada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom