Televisheni ya taifa China yasitisha matangazo ya mechi za La Liga kufuatia utani wa Mbappé

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Shirika la utangazaji la televisheni la China, CCTV, halikuonyesha mechi ya Real Madrid iliyochezwa Jumapili, licha ya mshambuliaji nyota wa klabu hiyo, Kylian Mbappé, kuomba radhi kuhusu matamshi yake aliyokiri kuwa hayakuwa ya busara kuhusu aliyekuwa kiongozi wa China, Mao Zedong.

Mbappé alikosolewa vikali baada ya kusema kuwa picha ya kuchekesha zaidi kwake ni ile inayoweka uso wake kwenye mwili wa dikteta wa China anayefanana na Mao.

China Media Group, ambayo ni mmiliki wa CCTV, ilitangaza Jumanne iliyopita kuwa itasitisha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, kufuatia malalamiko yaliyoibuliwa na kauli hiyo. Tukio hilo pia limesababisha baadhi ya kampuni za China kusitisha ushirikiano wao na Mbappé.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilisema imepokea kwa uzito ombi la radhi la Mbappé. Real Madrid na La Liga pia zimeomba radhi.

Awali, China Media Group ilikuwa imetaka pande zote tatu ziombe radhi, ikisema hilo lilikuwa sharti la msingi ili kuhitimisha suala hilo.

Shirika hilo limepokea maombi hayo ya radhi, lakini halijatoa maelezo kuhusu muda ambao kusitishwa kwa matangazo hayo kutaendelea.

Mbappé, ambaye anaripotiwa kutoa kauli hiyo alipokuwa akishiriki katika kipindi cha mazungumzo cha televisheni cha Ufaransa, The Bridge, aliomba radhi baadaye siku hiyo ya Jumanne.

“Kauli yangu haikuwa ya busara, na sasa ninaelewa kuwa iliwaumiza watu wengi nchini China na katika jamii za Wachina duniani kote,” alisema.

Utani huo haukupokelewa vizuri nchini China, ambako Mao anaheshimiwa na Chama cha Kikomunisti, licha ya kuhusishwa na moja ya vipindi vilivyogharimu maisha ya watu wengi zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Katika mechi ya Jumapili, Real Madrid iliifunga Racing Santander mabao 3 kwa 0. Mbappé, Jude Bellingham na Yan Diomande walifunga mabao hayo.
 
Na aliyechora hiyo katuni alichukuliwa hatua gani !?
Aliyemhoji mbape Hilo swali alichukuliwa hatua gani!?
Jamaa analazimishiwa makosa ili mwakani Dior nyingine waseme 'sio mstaraabu'
 
Dogo nae shule empty au Exposure ya dunia hana kabisa..Hili ni tatizo la GEN Z wengi sana kutokujua mambo ambayo watu wengi ulimwenguni wanayajua,mfano mpaka kasema neno DIKTETA WA CHINA ina maana alikuwa hajui kama huyo dikteta jina lake ni Mao Ze Dong mtu maarufu kabisa ambaye almost kila mtu anamjua..Niliwahi kuona Post moja tiktok AKON anaimba wimbo wake wa zamani wa Locked up GEN Z wakawa wanacomment kwa namna ya kutomjua kabisa AKON wengine eti wakawa wanasema Akon anatakiwa atoe huu wimbo,wengine wakawa wanasema AKON atakuja kuwa mchezaji mkubwa ni kama Ishowspeed tu kipindi kile alikuwa hamjui ARSENE WENGER ni nani,pamoja na sifa zote Arsene wenger alizoimbwa nazo
 
Wachina wana sheria kali, angalia hizi social platforms ambazo ziko blocked:
1000212501.jpg
 
Dogo nae shule empty au Exposure ya dunia hana kabisa..Hili ni tatizo la GEN Z wengi sana kutokujua mambo ambayo watu wengi ulimwenguni wanayajua,mfano mpaka kasema neno DIKTETA WA CHINA ina maana alikuwa hajui kama huyo dikteta jina lake ni Mao Ze Dong mtu maarufu kabisa ambaye almost kila mtu anamjua..Niliwahi kuona Post moja tiktok AKON anaimba wimbo wake wa zamani wa Locked up GEN Z wakawa wanacomment kwa namna ya kutomjua kabisa AKON wengine eti wakawa wanasema Akon anatakiwa atoe huu wimbo,wengine wakawa wanasema AKON atakuja kuwa mchezaji mkubwa ni kama Ishowspeed tu kipindi kile alikuwa hamjui ARSENE WENGER ni nani,pamoja na sifa zote Arsene wenger alizoimbwa nazo
Aisee waswahili hivi wewe ni kipi umemzidi mbape?
 
Information is Power
 
Back
Top Bottom