Mimi naamini business yoyote inahitaji uwe risk taker...so as long as it pays back mtaji wako na haichukui muda wako mwingi esp kama huna kingine cha kufanya, just go for it..hiyo dola 400 si nyingi kivile ya kufanya watu waogope..by the time hiyo pyramid scheme inacolapsi unaweza kuwa ushatengeneza kamtaji kako ka kufanyia business ingine. So fikiria kivyako zaidi usifate mkumbo....za mwenzio changanya na zako. Mimi binafsi sijawahi kuisikia but nikijua info zaid ntapata wapi ntatake risk.
Ni kama network marketing zingine, I mean foreverliving, oriflame, gnld, na questnet. Na wala sio kama DECI.. Mimi nilishawahi fanya kazi na questnet lakini nilishindwa kwa hiyo nina experience... Hii Yenyewe unanunua software yao ya VoIP ambayo unaiweka kwenye computer na itakuwezesha kupiga simu kwa kutumia pc kwenda kwenye pc au mitandao mingine kama vile kwenye skype kwa gharama nafuu sana. Ila pia ukishainunua iyo software ambayo ndo inauzwa package ya bei ya chini ni USD. 400 .. Sasa ukishaingia kwenye system hiyo unaweza kuwa unatangaza software yao kwa kupost Ads kwenye web yao... Unatakiwa upost mara moja kwa siku ambapo kwa wiki utapata USD 20 lakini kama ukiacha kupost hata kwa siku moja hiyo wiki nzima hutalipwa... Kwa upande mmoja mi naona hawa jamaa ni wazuri kulinganisha na makampuni mengine kama foreverliving ambapo utakuwa unapiga misele barabarani kuuza bidhaa na usipouza hupati. Kitu.. Ila hii unakaa kwenye laptop yako kama dakika 5 then umemaliza.. Ukiuza unapata chako lakini hata kama usipouza na ukawa unapost ile USD 20 iko palepale... Ni hayo tu.
Hii ni nzuri hasa hasa kwa wenye access ya Internet mana haihitaji nguvu nyingi kupata dola 20 kwa wiki ni swala zima la kujiwekea ratiba ya kila cku kwa dakika 5, ndani ya miezi 3 mpaka 4 utakuwa usharudisha pesa yako unaanza kula faida..Nadhani ni nzuri kuliko gnld ambayo nilishawahi kuifanya na kuiacha na nyinginezo..Mbali na hivyo itakuongezea hata ujuzi wa kutumia Computer..
Wapendwa wana JF hivi majuzi kuna watu wamekuwa wakiniuzi hii idea ya TELEX free ambayo imenifanya nijiulize maswali kadhaa ikiwamo je....hii kitu ni ujanja ujanja mwingine wa mjini au.Wataalamu munijuze kidogo.
Nawakilisha