Msafiri Travelers
New Member
- Dec 2, 2015
- 1
- 3
NJIA YA MARANGU -KUKWEA PAA LA AFRIKA
Marangu (Njia ya Coca Cola): Hii ni njia jadi na ya moja kwa moja miongoni mwa njia nyingi zinazoelekea mlimani. Ni njia yenye shughuli nyingi, na iliyosheheni vifaa muhimu na bora kuliko zingine. Kama utaamua kuitumia, ina maana kuwa watu wengine watakuwepo pamoja nawe, pia utapita kwenye vibanda vilivyo bora, muono mzuri wa kilele cha Mawezi, na bila shaka utakuwa na kampaniya kutosha. Kama utasafiri wewe, hii ni njia ambayo ni rahisi kujiunga na makundi kutoka sehemu nyingine na kutembea pamoja.
Siku 00 ? Kuwasili Moshi Wageni kuwasili Mjini Moshi. Watachukuliwa na kukupeleka hoteli waliyoichagua Mjini Moshi kwa ajili ya utambulisho wa na maelezo ya kupanda mlima kwa mara ya kwanza. Usiku watalala hotelini na kupata kifungua kinywa asubuhi ya siku inayofuata.
Siku 01: Safari ya gari kutoka Moshi mpaka Marangu kupitia Vibanda vya Mandara.Kuelekea geti la Marangu saa 3.30 asubuhi. Kutoka getini wageni watatembea umbali wa masaa 3-4 kupitia msitu wa mvua wa mandara na kuona vitu vya kupendeza machoni kisha wataelekea katika vibanda vya Mandara vilivyipo kwenye muinuko wa futi 9000 kutoka usawa wa bahari, karibu na Kreta ya Maundi,ambapo watapata chakula cha mchana na jioni.
Siku 02: Mandara mpaka vibanda vya Horombo.
Wageni wataelekea kupanda vibanda vya Horombo na kuelekea kupitia msitu wa mvua ndani ya uwanda wa nyasi.Umbali wa kutembea hadi kufikia vibanda vya Horombo ni futi 3,720m (12,200ft)kutoka usawa wa bahari hii ni kama 14km na masaa 5-7 kufikia vibanda vya Horongo na kupata ,kifungua kinywa,chakula cha mchana na jioni na mahali pa kulala .
Siku 03: Horombo mpaka vipanda vya Kibo.
Kutoka vibanda vya Horombo mpaka Kibo ni futi (15,430) 4,703m kutoka usawa wa bahari ambazo ni 13km na masaa 6-7 kufikia bonde la mwisho la maji katika vijia vya milimani,nakupata kifungua kinywa,cha kula cha mchana ,cha jioni na mahali pa kulala.
Siku 04: Kibo mpaka Uhuru kushuka vibanda vya Horombo.
Jaribio la kufikia kilele haunza muda mfupi baada ya siku wa manane. Kwa muda wa masaa 5, mmoja anapanda sehemu yenye mteremko mkali zaidi kwenye njia ya Gilman na hutumia futi 18,640 juu ya mdomo wa kilele, na dakika 45 zilizobaki kuelekea sehemu ya juu zaidi, UHURU PEAK ambayo ni rahisi. Na uchovu wa usiku unaishia katika vibanda vya Horombo kwa kifungua kinywa ,chakula cha mchana pamoja na jioni.
Siku 05: Horombo mpaka Marangu getini kurudi Moshi.
Kuelekea katika vibanda vya Mandara mpaka makao makuu ya mbuga ambapo waandaji waliofanikiwa wanapokea vyeti vya vya kufanikiwa. Baada ya hapo kurudishwa Moshi hotelini kwa ajili kwa usiku mmoja, kitanda na kifungua kinywa.
Siku 06: Baada ya kifungua kinywa, kurudi nyumbani au sehemu nyingine.
Mwisho wa Huduma.