CORAL
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 2,813
- 1,827
Tembo mmoja huko Zimbabwe ameacha watu midomo wazi baada ya kutafuta madaktari wa wanyama pori wamtibu kufuatia jeraha alilopata kichwani kwa kupigwa risasi na majangili.
Majangili walimpiga risasi tembo huyo wakitaka kumuua ili wang'oe meno yake wakauze. Lakini tembo huyo alinusurika na kuwatoroka majangili.
Cha kushangaza akaanza mara moja safari ya kuwatafuta waganga wa kuponya jeraha la risasi ili aepuke maumivu makali aliyokuwa nayo.
Madaktari wa wanyamapori walipomuona anakuja kwa mbali akitembea taratibu hawakujua hasa alikuwa anataka nini.
Waliwaza kuwa huenda wapo kwenye himaya yake na anataka kuwafukuza au huenda anadadisi tu kujua wanafanya nini pale.
Walijiweka tayari kukimbia kwenye gari lao ikiwa lolote litatokea. Wakasubiri akazidi kusogea. Alipokaribia zaidi ndipo wakagundua kuwa ana jeraha kichwani. Sasa wakajua kuwa maisha yao hayakuwa hatarini bali maisha ya tembo.
Wakaanza kumhudumia mara moja wakamchoma sindano ya ganzi na kisha kumfanyia upasuaji na kuitoa risasi kichwani. Wakampa tiba na kumruhusu. Tembo huyo alianza kuondoka bila kupaniki na kuelekea porini na alipofika kwenye mti fulani akajiegesha na kulala usingizi.
Maswali yaliyowasubua madaktari hao ni kwamba:
1.Huyo tembo baada ya kupigwa risasi aliwezaje kudumisha utimamu wa akili na kufanya maamuzi sahihi ya kutafuta tiba?
2. Baada ya kujeruhiwa na majangili tembo huyo aliwezaje kutofautisha madaktari na majangili? Yaani nini kilimuaminisha kwamba si watu wote ni wabaya kuna watakomuonea huruma na kumsaidia?
Yaani ni ajabu kweli
Elephant Walks Up to Vehicle Asking for Help after being Shot by Poachers