Tembo wamekuwa tishio kwa wananchi, Serikali iwavune kwa Usalama wa Raia

Tembo wamekuwa tishio kwa wananchi, Serikali iwavune kwa Usalama wa Raia

Maisha ya mwanadamu kwa asili yake ni kupambana na changamoto. Utatuzi wa changamoto moja, huzaa changamoto nyingine. Udhibiti wa ujangili umezaa changamoto hii. Kwa kawaida, asili inayo namna yake ya kujidhibiti. Suluhu sio kuwavuna, bali ni kuanzisha kilimo cha pilipili na ufugaji nyuki. Hapo wakazi watakuwa wametengeneza buffer zone. Tusiwe na ufumbuzi wa kiharibifu.
Umenena vyema lakini changamoto ni nyingi, kilimo cha pilipili kinapunguza kwa kiasi kidogo sana hasa wakati pilipili zimekomaa. Tembo mmoja ana uwezo wa kula kilo mia kwa siku bado maji na madini. Idadi yao inavyoongezeka na wenyewe inabidi waende mbali zaidi kutafuta mahitaji muhimu. Maeneo mengi ya uhifadhi yamejitenga kama visiwa hakuna movement ya wanyama pori kutoka sehemu moja hadi nyingine. Ongezeko la makazi kwenye maeneo ya wanyama wildlife corridors, ndio chanzo cha mifarakano kati ya wanyama na watu.
 
Back
Top Bottom