Temeke, Dar: Mwenyekiti wa Mtaa aliyepita bila kupingwa mbaroni kwa tuhuma za wizi wa Tsh. Milioni 12

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mwenyekiti wa Mtaa wa Changanyikeni Kata ya Toangoma katika Wilaya ya Temeke kwa tiketi ya CCM, Suzanne(Dionisia) Kamugisha amekamatwa akidaiwa kuiba Tsh. 12,000,000/-. Mruhumiwa na wanae wawili wsnashikiliwa kituo cha polisi Mbagala.

Inadaiwa juzi, mwanaye aliyeajiriwa katika duka la simu-pesa alikutwa na hasara ya Tsh. Milioni 12 alipohojiwa alimtaja Mama yake (Suzanne) kuchukua fedha hizo kwa ajili ya kampeni uchaguzi wa ndani wa chama

Viongozi wa Kata hiyo (Diwani, Mtendaji wa Kata na Katibu Kata kupitia CCM) tangu asubuhi ya leo wanashughulikia kumtoa rumande bila mafanikio

Aidha, katika hatua nyingine inadaiwa Wananchi wa Mtaa huo wameanza kuhamasishana kupiga kura ya kutokuwa na imani naye kwenye mkutano wa Mtaa


Wananchi na hata makada wa CCM wanasema hawamtaki kabisaa.

Huyu pia anatuhumiwa kukwapua milioni 23 za VICOBA halafu akakingiwa kifua na Uongozi wa Kata asipatwe na mkono wa sheria.

Bahati mbaya hiyo hela aliitumia kuwanunua viongozi wa Tawi na Kata kisha akapitishwa kinguvu.

Makada wa CCM walijiandaa kuupigia kura upinzani ili iwe funzo lakini ikala kwao baada ya mama huyu kupitishwa bila kupingwa.
 
Wenyeviti wa viyi maalumu.. Sasa kampeni walifanya lini wakati Ccm iliwafanya wote biti maalum?
 
Ni mijizi tupu kumbe!! yanaenda kwa baba yao baba wa ujambazi!! Jogoo hajawika
 
Huyo bi mkubwa nae bati kweli yani!ss jaksi yote hiyo kwa ajili ya uenyechair,je ingekuwa ubunge ingekuwaj!? anyway CCM mbele kwa mbeleee...🚶🏿🚶🏿🚶🏿
 
Ki ujumla madahaifu ya mtu hayatokani na chama, ila ni ya mtu biafsi.

Si vizuri kumuunganisha moja kwa moja na chama cha ccm. Ila mahusianao ya wizi huo na chama yatajitokeza tu pale wanachama watatumia nguvu ya chama kumtetea.
 
Ki ujumla madahaifu ya mtu hayatokani na chama, ila ni ya mtu biafsi.

Si vizuri kumuunganisha moja kwa moja na chama cha ccm. Ila mahusianao ya wizi huo na chama yatajitokeza tu pale wanachama watatumia nguvu ya chama kumtetea.
Kasema alichukua pesa kufanyia kampeni ndani ya chama au hukuona hiyo paragraph?!
Pesa inafanyaje kampeni ndani ya chama kama siyo rushwa?!
Kwanini hakwenda kukopa bank ?!
Utapeli ni wizi,.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…