Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mwaka 2010 alikuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Temeke kupitia CUF, kutokana na kutofutwa kwa demokrasia, na uchaguzi huu alikuwa mgombea Ubunge Jimbo la Temeke kupitia CHADEMA.
Kutokana na kuwa Demokrasia ndani ya Vyama vya Upinzani haipo, leo ameamua kujiunga CCM
Amejiunga katika mkutano wa Mgombea mwenza wa Urais, Samia Suluhu, Kigamboni Dar-es-Salaam
======
Dare es Salaam.
Aliyekuwa Mtia nia kutaka kugombea Ubunge Jimbo la Temeke kwa Tiketi ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) Lucas Limbu amtangaza kukihama Chama hicho na kuhamia Chamaa cha Mapinduzi (CCM) kutoka na kile alichodai kuwa kukosekana kwa Demokrasia ya kweli ndani ya Chama hicho.
Limbu ametoa kauli hiyo leo Jumanne Septemba 8 katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi Jimbo la Kigamboni mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliyefika kuzindua rasmi Kampeni hizo.
Amedai kuwa Vyama vya upinzani vinajaribu kufanya kampeni huku wakijuwa kuwa lengo lao ni kutaka kuwa na idadi kubwa ya wabunge wakiwemo wale wa viti maalumu ili baadae waweze kupata ruzuku kutoka Serikalini kutokana na nafasi za viti vya ubunge walivyopata.
“Nimeamua kuondoka CHADEMA kutokana na kukosekana kwa Demokrasia ndani ya Chama, Makamu Mwenyekiti Bara ambaye pia ni mgombea wa Urais wa Chama hicho Tundu Lissu antangaza kutaka haki huku ndani ya Chama hakuna haki wala Demokrasia” amedai Limbu.