KERO Temeke: Shule ya Msingi Vikunai, wanafunzi wanakaa chini na kutozwa Tsh 500 kila siku kwa madarasa ya mitihani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Shule ya ,singi Vikunai iliyopo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam kuna changamoto kubwa Wanafunzi hawana madawati baadhi wanakaa chini.

Shule pia inabebesha wazazi mzigo wa kutoza Tsh 500 ya mtihani kwa madarasa ya mitihani, hiyo tsh 500 mwanafunzi anatakiwa kwenda nayo kila siku, hivyo ni mzigo kwa wananchi wa hali ya chini

Mwanafunzi asipopeleka Tsh 500 anachwapwa jambo ambalo si sahihi, wananchi wanalalamika kwenye mikutano ya Serikali za Mtaa lakini hakuna mabadiliko. Serikali isifumbie macho sUala hili madhara yake ni makubwa .
 
Atleast wewe umekuwa na guts la kuliongelea hili jambo wenzako wanaamini ni dhambi, mtanzania inabidi usifie serikali.

Sikutegemea kwepo kwa hili tatizo bado kwa mkoa wa Dar Es Salaam, niliamini upande wa afya ndiyo kuna madudu zaidi
 
Hii ni aibu,walimu Tamaa imezidi,wananchi wenyewe mlo mmoja tabu hiyo 500 kila siku wanatoa wapi?na mitihani gani hiyo ya kufanya kila siku shule haina mbao kama ni mazoezi?,usaw huu bado kuna Halmashari mtoto anakaa chini kweli,serikali msifumbie macho hili ni Aibu
 
Atleast wewe umekuwa na guts la kuliongelea hili jambo wenzako wanaamini ni dhambi, mtanzania inabidi usifie serikali.

Sikutegemea kwepo kwa hili tatizo bado kwa mkoa wa Dar Es Salaam, niliamini upande wa afya ndiyo kuna madudu zaidi
Umeshathibitisha kuwa kilichosemwa ni ukweli?
 
Kuna watu wanaimba wimbo wa Ubaya wa English medium kila siku, kumbe wanajifariji uvivu na umaskini wao
 
Halafu anaibuka hohehohe mmoja anakuambia EMs ni kupoteza pesa!
116096.png

unasemaa?!?
 
Shule ya msingi Vikunai iliyopo manispaa ya Temeke jijini Dar Salaam kuna changamoto kubwa wanafunzi hawana madawati baadhi wanakaa chini.

Shule pia inabebesha wazazi mzigo wa kutoza Tsh 500 ya mtihani kwa madarasa ya mitihani, hiyo tsh 500 mwanafunzi anatakiwa kwenda nayo kila siku, hivyo ni mzigo kwa wananchi wa hali ya chini

Mwanafunzi asipopeleka tsh 500 anachwapwa jambo ambalo si sahihi, wananchi wanalalamika kwenye mikutano ya Serikali za Mtaa lakini hakuna mabadiliko. Serikali isifumbie macho sUala hili madhara yake ni makubwa .
Sasa Kuna shida gani mwanao akitoa Tshs 500 Kila siku akipigishwa paper na kusaishiwa
Hivi nyinyi wazazi wa uswahilini mna shida gani kwanini hamtaki kuwekeza elimu Kwa watoto wenu
 
Cha ajabu unaweza kuta 20% ya wazazi wa watoto kwenye hiyo shule wako humu lakini hawajawahi kuongelea hata siku moja hilo tatizo, wakiamini ni dhambi,kinyume na sheria, mwananchi wa kawaida inabidi wateseke.
 
Shule ya msingi Vikunai iliyopo manispaa ya Temeke jijini Dar Salaam kuna changamoto kubwa wanafunzi hawana madawati baadhi wanakaa chini.

Shule pia inabebesha wazazi mzigo wa kutoza Tsh 500 ya mtihani kwa madarasa ya mitihani, hiyo tsh 500 mwanafunzi anatakiwa kwenda nayo kila siku, hivyo ni mzigo kwa wananchi wa hali ya chini

Mwanafunzi asipopeleka tsh 500 anachwapwa jambo ambalo si sahihi, wananchi wanalalamika kwenye mikutano ya Serikali za Mtaa lakini hakuna mabadiliko. Serikali isifumbie macho sUala hili madhara yake ni makubwa .
CCM Hoyeee
 
Back
Top Bottom