KERO Temeke: Shule ya Msingi Vikunai, wanafunzi wanakaa chini na kutozwa Tsh 500 kila siku kwa madarasa ya mitihani

KERO Temeke: Shule ya Msingi Vikunai, wanafunzi wanakaa chini na kutozwa Tsh 500 kila siku kwa madarasa ya mitihani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Madarasa ya mitihani yamegeuzwa fursa shule za msingi nyingi ........ Hili la kukaa chini ni aibu Sana ni Kama siamini Eti mjini bado watoto wanakosa madawati loh...
 
Shule ya msingi Vikunai iliyopo manispaa ya Temeke jijini Dar Salaam kuna changamoto kubwa wanafunzi hawana madawati baadhi wanakaa chini.

Shule pia inabebesha wazazi mzigo wa kutoza Tsh 500 ya mtihani kwa madarasa ya mitihani, hiyo tsh 500 mwanafunzi anatakiwa kwenda nayo kila siku, hivyo ni mzigo kwa wananchi wa hali ya chini

Mwanafunzi asipopeleka tsh 500 anachwapwa jambo ambalo si sahihi, wananchi wanalalamika kwenye mikutano ya Serikali za Mtaa lakini hakuna mabadiliko. Serikali isifumbie macho sUala hili madhara yake ni makubwa .
itakua ela ya kiwi iyo maana mbuzi anakulaga alipofungwa
 
Hata huko Mkuranga na Rufiji, watoto wanalipishwa 4000 kwa mwezi kwa ajiki ya mitihani, na ni darasa la 4 na darasa la 7.
4,000 kwa mwezi si sawa na 500 kwa kila siku kama mwandishi alivyoandika.
Ama nawe unaona hiyo 4,000 kwa mwezi ni kubwa?
 
Back
Top Bottom