TEMESA wakubaliana na Azam Marine kuvusha abiria Kigamboni (Ferry)

Mm naunga mkono wawekezaji wenye nia njema,uzuri wa bakhresa hana janja janja kwenye biashara zake,anapata faida kwa kuzingatia ubora wa bidhaa zake,mi sijakutana na mtu analalamikia ubora wa bidhaa zake,mnyonge mnyongeni haki yake mpeni,tukiwakataa wazawa ambao wameajiri ndugu zetu mnataka muwekezaji atoke nchi gani??

Kama anaweza apeww jumla apeww guarantee ya soko ili aletw vivuko vya uhakika,kwa sasa hawez kuinvest sababu vivuko siyo andazi kwamba ukishindwa kuliuza utalitafuna mwenyewe,kivuko unaleta uwe na uhakika wa biashara
 
Kuna baadhi ya huduma zinapaswa kutolewa na serikali, mfano hiyo ya kivuko. Serikali kushindwa ni dalili mbaya
Kusema tuwape wazawa kufanya biashara kwenye huduma zinazopaswa kutolewa na serikali ni hatari.
Hapo ni sawa na kusema hospital Kama muhimbili pia tuwape wafanyabiashara waiendeshe
 
Sijui niseme nini mkuu 'Yoda', nitaisoma kwa utulivu nione ninachoweza kuchangia.

Lakini niache neno hili: "huu ni mfano mzuri wa serikali kushindwa kufanya biashara"?

Mbona kila siku inafanya biashara na wafanya biashara? Jibu hili nikilipata labda utakuwa ndio mwanzo kwangu kufunguka akili juu ya mambo haya!
 
Serikali huwa haiwezi kufanya biashara,ikijaribu huwa ni majanga tu,hili lilibidi liwe limefanyika zaidi ya miaka kumi iliyopita,sasa hv mazingira yamelazimisha tu,serikali inatakiwa ibaki katika uratibu wa hizi public service,kwa wenzetu hata magereza umirikiwa na watu binafsi.maswala ya serikali kushikilia njia za uchumi,yabaki kwenye sekta nyeti zenye kuitaji mitaji mikubwa na mikataba ya nchi na nchi,
 
CAG na PCCB hebu tieni mguu Temesa kukagua mikataba dhidi yake na Sighman Safari Haulage juu ya ukodishaji majengo VS sheria ya manunuzi
 
Serik
Hapana serikali kutoa huduma za vivuko,ni makosa,wao wabaki katika kuratibu tu,zama za serikali kufsnya biashara zilishapita,miaka ya 80,90,kulikuwa na maduka ya serikali ya kuuza sukari,unga,chini ya NMC(national milling corporation)hebu fikiria nikiwa mdogo unatoka liverside mpaka ubungo mataa kuwahi gari limekuja kuuza sukari!,yaani mtaani. Hakuna aliyekuwa anaruhusiwa kuuza sukari,unga,ni maduka ya serikali tu,unapanga foleni kununua unga!!ulikuwa upuuzi wa sera za kijamaa.
Yaani kweli kwenda Zenj,tusubili boat za serikali?serikali iweke mazingira,incentive kuvutia watu binafsi wawekeze kwenye hizi huduma.
 
Haya ndiyo uliyojifunza ndani ya vitabu, na hukutaka kujiongeza ukapanua akili kuona kwamba hakuna sababu kwa nini serikali isifanye inachotaka kufanya kwa ufanisi?
Huna maelezo yoyote unayoweza kuweka hapa, kwa nini mfanya kazi serikalini asifanye kazi yake kwa ufanisi kama yule aliyeko kwenye shughuli binafsi!

Halafu hapo juu unalalamika na "sera za kijamaa", na kutoa mfano wa maduka ya kuuza sukari? Huna 'context' nyingine yeyote ya kukueleza hayo matukio yalikuwa yamelazimishwa na kitu gani, ila "sera za kijamaa"? Huo ndio ujamaa unaoujua wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…