The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Binafsi ningependa ufafanue ili tukuelewe..Kumb. 18:18_22
Imeeleza sifa za mtu aliyetumwa na Mungu.
TB. Joshua hajatumwa na Mungu.
Ni ukweli mchungu.
Ni ishara gani kumhusu TB. Joshua zinazom - disqualify asiwe mjumbe wa kweli wa Neno la Mungu (Nabii) na kukufanya uje na hitimisho hili..?
Nimesoma andiko hili ulilokwoti. Kwa faida ya wote naomba niweke mistari hiyo hapa:
Kumbukumbu la Torati 18: 18 - 22
"..18 Mimi nitawandokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. 19 Hata itakuwa mtu asiyesikiliza maneno atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake. 20 Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena kwa jina la miungu mingine, nabii yule ATAKUFA. 21 Nawe ukisema moyoni mwako, tutajuaje neno asilonena BWANA? 22 Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilonena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope..."
Sasa ungedadavua vizuri muktadha wa mistari hii ya Biblia namna inavyohusika na hoja yako kisha inavyopatana au kupingana na karama ya unabii aliyokuwa nayo TB. Joshua, ningegurahi sana binafsi kujifunza kutoka kwako..