Mwisho wa siku Biblia itabaki kuwa kweli kwa wanao iamini na vile vile itabakia kuwa upuuzi kwa wasioamini. Hii ndiyo maana ya imani (you believe/trust what makes sense to you). Mambo ya Mungu yako vile, kila mtu anaguswa kwa namna yake na kwa maana inayoeleweka kwake.
Imani inahitaji kujifunza unyenyekevu - "intellectual humility" na kuacha kiburi - "dry intellectualism". Ni dhahili kuwa kuna vitu tunavyovijua na tunaweza kuvielezea kwa ufasaha. Lakini pia kuna vitu tusivyovijua tunahijaji imani/trust kuvipokea. Hapa nina maana ya reasonable/responsible faith (believing because it makes sense in all circumstances that something is true) na siyo fideism (blind faith).
Tunapoanza urafiki na mtu fulani kwa vile hatuoni undani wa huyo mtu na jinsi urafiki wetu utakavyoenda (yaani hatuna empirical proofs za kujua alivyo A-Z) huwa tuna amini kuwa anachosema ni kweli au siyo kweli (depending on how we geuninely perceive the nature of our relationship).
Mtu akitaka kuoa au kuolewa kwa vile hamjui mwenzake kikamilifu huwa ana trust/believe kuwa mwenzake huyo ndiye anataka awe mume/mke wake na kutokana na imani hiyo, wanakaa pamoja kama mume na mke na kujenga familia yao. Trust inakuja pale ambapo kuna certainity either by intuition or experience of the nature of the relationship.
Kuna mambo mengi yanayoonyesha nafasi ya imani katika maisha yetu - ikiwa ni pamoja na kuamini kuwa tukiwa kazini familia zetu ziko nyumbani au kwamba tukifanya kazi kwa bidii tutafanikiwa katika maisha yetu.
Hapa tunahitaji imani kwa vile licha ya kuwa hatuwezi kuthibitisha kuwa mtu akifanya kazi kwa bidii atafanikiwa tumeng'amua (beyond reasonable doubts) kwamba ni kweli tukifanya hivyo. Faith is born out of doubts - what our intelligence accepts but fails to see clearly how and where it ends. There faith takes over.
So, faith is just a step beyond what I can genuinely reason and comprehend but it's linked to reason in the sense that what I believe must make sense to me personally. It may not, however, make sense to others at the same time because faith is a gradual journey and personal commitment.
Kwa hiyo, imani inahusu maana nzima ya uwepo wetu hapa duniani na hatima ya maisha yetu kama sisi lakini pia kama jamii na binadamu wote kwa ujumla.
Narudia tena mambo ya imani huwezi kuyathibitisha kama vile unavyoweza kuthibitisha kuwa 'mjusi' au mmea fulani ni kiumbe hai (bio) au ukichemsha maji yanakuwa mvuke. Mambo ya imani yanathibitishwa na jinsi mtu mwenyewe alivyoguswa na kuishi. "The heart has reasons the mind cannot understand," said Philosopher Pascal. Faith is about trusting/accepting what is beyond what's commonly known/perceived.
Darwin, unachojaribu kufanya wewe kinaitwa 'scienticism'. Yaani, una'force' science iielezee imani wakati haiwezekani. Sasa kufanya hivyo siyo kufanya kitu scientifically either. You cannot simply break scienfic rules and claim what you are doing is scientific; you are not!
Ukitaka kuongelea faith, ongelea metaphysics, ontology - what's beyond observable reality. Kwa vile hapa ndipo unapoweza kuielezea faith jinsi ilivyo. Na caterories zako za thinking lazima pia ziwe about things beyond empirical proofs.
Mind you, science haielezi kila kitu hapa duniani na wewe unataka kusema kuwa inaweza. Kuna disciplines zingine ambazo ziko 'well equipped' with tools of explaining 'faith' or the spiritual world but not science.
Mfano, should we say that what we don't know (what we haven't seen, touched, smelt, heard, tasted) doesn't exist?
Kuhusu Biblia, narudia: Ni Neno la Mungu - which was communicated orally and at a later stage was preserved in written form - lilielezewa na kuandikwa na binadamu, linaelezewa kibinadamu na kwa lugha ya kibinadamu. Kuonyesha hali hii ya kibinadamu, Biblia ina karatasi kutoka viwandani; imechapishwa na binadamu na imesanifiwa na binadamu na lugha imehaririwa na watu kulingana na mazingira yao na matumizi ya lugha, mila na desturi zao. Biblia ni neno la Mungu kupitia mikono ya kibinadamu.
Lakini pamoja na haya yote, Biblia inahusu ujumbe wa Mungu kwa binadamu na hatima yao. Inatumia lugha ya picha, nahau, methali, mifano na misemo katika kuwasilisha ujumbe wake. Mungu anaonyesha uwezo wake kupitia binadamu.
Ni kama creation narratives kwenye Kitabu cha Mwanzo zinaelezea Mungu kuwaumba wanadamu kwa kutumia udongo (anthropomorphism). Did it really happen that way? No. The stories want to convey a message of relationship between God, humans and creation (the universe).
Biblia inaelezea pia fadhila zinazomfanya binadamu awe mwadilifu na kuishi na binadamu wengine kama ndugu. Na ujumbe wake ni wa muda wote, mahali pote na kwa watu wote. Neno la Mungu ni Neno la uzima: it's dynamic na ni la waktai uliopita, wa sasa hata ujao na milele yote.
Vitabu vya historia vinaelezea matukio ya binadamu kutoka kizazi kimoja kwenda kingine na namna walivyokabiliana na mazingira yao. Vitabu vya bailojia vinaelezea viumbe hai na tabia zao. Lakini hatima binadamu na matarajio yao hayaelezwi na vitabu kama hivi.
Neno la Mungu/ujumbe wa Mungu unatoa changamoto katika maisha na namna ya kuyabadili ili yawe ya kumpendeza Mungu. Na bila kulitafakari hilo neno la Mungu hatuwezi kupata ujumbe wake. Neno lolote linalotuasa kufanya au kuacha kufanya kitu fulani lazima tulitafakari na kulifania discernment.
Vinginevyo hatupati ujumbe wake. Darwin wewe hauitafakari Biblia unaikariri tu na kwa kufanya hivyo, na kwa vile unachukua vifungu kadhaa out of context, lazima uwe na maswali kama uliyo nayo kwani huna imani na hivyo kuisoma kwako ni kazi bure. Biblia ni kitabu kinachohusu imani na siyo sayansi, civics au bailojia. Hivyo usomaji wake pia ni wa kiimani - unasoma sura au mstari fulani na unatafakari ili upate maana yake.
Lakini wewe ukisoma: 'Mungu aliumba dunia siku sita na ya saba akapumzika' unaona ni kweli siku zenyewe ni Jumatatu hadi Jumamosi na ile ya saba Mungu alipumzika kweli; ukisoma 'Yona alikaa ndani ya samaki siku tatu' unaona ni kweli alimezwa na samaki na baada ya hizo siku tatu samaki akamtema tena. Kusoma Biblia kwa namna hii hakumpi msomaji ujumbe wake. Ndiyo maana njia nzuri ya kusoma Biblia ni kufanya exegesis au hermeneutics ili kujua kitu gani kiliandikwa kwa nani, kwa nini na kwa maana gani.
Hayo uliyojiandaa kuyaleta yalete tu. Hakuna anayeyaogopa kwani kupinga kitu fulani siyo sababu kuwa kitu fulani siyo kweli wakati mwingine kunaonyesha tu uelewa mdogo wa mhusika mwenyewe. Actually, kupinga kitu hakumaanishi kuwa kitu fulani si sahihi basi kunaonyesha kuwa mtu fulani ama ameelewa vingine au hana habari za kutosha kuhusu kile anachokipinga kama unavyofanya wewe.