Unapomuandika Newton, huwezi ukamuacha Robert Hooke.
Huyu jamaa na yeye, looohh, sijui nianzie wapi.
Kwenye Magari, majengo, Vyuma, Strength of Materials na takataka kibao ambao HOOK'S Law huwa inatumia, huyu jamaa ndipo unamvulia kofia. Katika maisha walikuwa hawapendani KABISAA na Isaac Newtons. Walikuwa wakishindana na kuibiana vitu walivyogundua. Huyu jamaa aliweka hii Graph ambayo hadi kesho itaendelea kutesa. Wahandisi wengi saana huwa inabidi kila kukicha wamtumie huyu jamaa. Binadamu pia tuna apply ugunduzi wake bila kufahamu.
Kusema ukweli, wako wengi sana ambao kila siku tunatumia ugunduzi wao. Sijui yupi ni muhimu au maarufu zaidi ya mwingine.