Kufukuzwa Kwa Ten hang ni suala la mda mtu, January hatoboi
KUTOKA DM KWA MDAU WA MAN U
UKWELI MCHUNGU TEN HAGG KOCHA WAKAWAIDA
Najua wengi mtabisha na kukejeri ila Ten hagg hawez kutufikisha popote ,Ni kocha WAKAWAIDA Sana
Timu inacheza kwa kuvizia , timu bado haijafikia hata kiwango alichofikia Ole Gunnar, huyu Sasa Ndiye alikuwa anacheza ile pure kaunta Attack
Ten hagg tuliingia Chaka , pale Ajax Wana falsafa yao hata akienda Mourinho lazima afate kucheza total football ,
Ten hagg dirisha moja katumia £250m Cha ajabu timu inashinda kwa kukaa nyuma, mpira wa hivi utaumbuka tu, tulimfunga Liverpool mwenye Majeruhi 8, lakin mpira alituzidi, tukamfunga Leicester, Southampton kwa tabu huku kipind Cha pili tukikaa nyuma dhidi ya timu dhaifu
Tukamfunga Arsenal kwa staili ya ujanja ujanja huku tukipigiwa mpira mkubwa nyumban kwetu , hii inatosha kuonesha huu mpira wa ujanja Tutaumbuka tu huko MBELENI
Unapotumia £250m kocha mwenye mbinu timu itaonekana tu inavyosakata kabumbu, Angalia Brighton wametuzidi Nini lakini hawachez kwa kuvizia
Ole Gunnar alikuwa akicheza na timu za kawaida anazitawala ,timu kubwa atazifunga kwa Kaunta halisi ile ya Ferguson,
Huyu Ten hagg mnasema apewe muda ,sawa labda kila dirisha aendelee kupewa £250m had ifike £1Billions labda tutaona timu ikicheza mpira
Ole Gunnar aliingiliwa kusajiri akaletewa Ronaldo ambaye hakumuhitaji, timu ikayumba wakamtimua
Ten hagg kimbinu tutasubiri Sana, tusubiri miujiza tu ya kushinda kwa kubahatisha
Kuna watu wanasema kipind Cha pili dhidi ya man City tulicheza , wanasahau man city alishashinda na ana mech ya UCL kesho, pia mwez wa 10 Kuna mech kila Baada ya siku 3,
Kama Pep Guardiola asingefanya Zile sub tungeogelea magoli mengi Sana
Ten hagg Ni kocha wa kawaida,. Tutakuja hapa kutaka afukuzwe , dirisha moja kashatumia £250M na timu inacheza kwa kuvizia
Klopp mwaka 2018 alipewa £177.5m akaleta watu wa maana ndiyo Liverpool hii iliyosumbua misimu karibu mitatu
Pep Guardiola msimu wa pili alitumia karibu £200m ,timu ikaanza KUPAMBANIA mataji
Arteta mwaka Jana alipewa £150m timu ikaanza kucheza vzr sio kuvizia
Ten hagg dirisha moja kapewa £250m anataka timu icheze kwa uviziaji, hautafika popote
Tuchel alitumia £250m dirisha hili, akaanza kucheza ovyo, katupiwa virago