6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Vipi wakuu, kwema huko mitaani.
Ebwana inasikitisha kuona nchi kubwa kama TZ, iliyosheheni watu wenye vipaji mbali mbali vya uigizaji, anakosekana mtu wa kuziba pengo aliloacha hayati Kanumba.
Mwanzo mwanzo Rey alikuja na mikwara ya kujifanya kuwa yeye ndo mwenye uwezo wa kuliziba na kulifunga kabisa pengo hilo, lakini baada ya miaka miwili ya mikwara tukaja kuona jamaa chali, kaangukia kichwa huku miguu ikiwa juu.
Wakaja wengine ambao nimewasahau mpaka majina, lkn na wao wakaangukia pua na kidevu.
Hakika jamaa alikuwa amebarikiwa kipaji cha pekee kabisa. Laiti angekuwa hai leo hii basi Tanzania tungekuwa na mastaa wakubwa sana walioshindikana Afrika mashariki ambao ni Kanumba na Diamond.
Bora kwenye mziki kidogo Diamond anapata chalenge ya kufukuziwa na kina Kiba, Harmoniza nk, lkn kwa Kanumba pamoja na kufariki ila amekosa hata wa kumsogelea karibu yake achilia mbali kuziba pengo lake.
Wakuu toeni ushauri nini kifanyike ili apatikane wa kusimama nafasi ya hayati Kanumba, maana kwa upande wa comedy naona Joti kafanikiwa kuziba pengo la mzee Majuto.