Ten years now, tasnia ya movie imekosa mbadala wa Kanumba nchini

Ten years now, tasnia ya movie imekosa mbadala wa Kanumba nchini

Hakuna Tasnia iliokosa mtu, sema utandawazi umebadilisha mambo, hata huko majuu hakuna movie zina kiki kama kipindi cha kina Rambo na Jack chain,
Now kila mtu ni celebrate kila mtu ni actor na comedian, hata angekuepo angepotea vile vile.
Swadakta mkuu. Kilichombeba Kanumba ilikuwa ni kukosa mbadala na kutokuwepo na njia za kumlinganisha. Ni kama vile mtu uwe unamiliki shati moja tu, utake usitake ni lazima ulipende. Ila pale utakapopata lingine hilo moja utaliona la zamani.

Leo hii sababu ya utandawazi na uwepo wa mbadala hata huyo Kanumba angeonekana kituko tu. Mfano mzuri leo hii ukiangalia movie za Kanumba aibu unaona wewe mtazamaji. Kwa kifupi hakuwa na ubora wowote bali alikuwa na fursa ya kuonekana pasi na kuwa na ushindani.
 
Wapo waigizaji bora kuliko yeye kwa sasa mfano akina luka wa maria. Jamaa anacheza characters tofauti za zote anaziweza. Uwa sipendi filam za bongo ila siku hizi kuna wanaonibamba. Kuna tamthlia moja nataman kuiona kaigiza mombasa kama shujaa fulani hivi hata sikujua kama ni yeye
 
Back
Top Bottom