MALKIA WA TABASAMU
Member
- May 23, 2024
- 15
- 43
Nimekutana na rafiki yangu wa kitambo kwa ghafula. Ni mahala ambapo hata ndotoni hakuna kati yetu ambaye angeamini kama tungekutana baada ya miaka 13 ya 'tusitambuane'.
Ilikuwa miaka ya ujana mbichi wenye utoto ndani yake. Alinipora "Shilingi niloithamini kabla hata sijaonja kuitumia" zingatia shilingi;
Moja ya kitu sijawahi kupigania ama kupambana sana nisikipoteze ni 'SHILINGI' Ni kiapo changu cha utoto kinacho 'make sense hadi leo.
Turudi kwangu na bishost!
Nilikutana naye stendi ya basi kitambo hicho, alikuwa kajiinamia, hakuna aliyemsemesha wala kujali hali yake. Mpenda hekaheka mie, kwenye mchaka mchaka wangu wa jioni baada ya jua la utosi lililomalizikia usogoni kwangu; nilipomuona nikamfuata. Nikajaribu kumsemesha bila mafanikio ya kusikia japo sauti yake.
Sikukata tamaa, nilimgusa na hapo nikabaini alikuwa akilia. Nilimsemesha na baada ya kutumiwa na Mungu kumkomboa akiwa katika hatua za mwisho kuelekea kuwa mama, aligeuka na kuwa jukumu langu. Mtoto hakuwa rizki, nyumbani alifukuzwa shauri ya ujauzito wake wa utotoni, mwanaume aliyemtundika jukumuni katika umri mdogo, alimkimbia. Niliishi naye. Nilimuingiza kwenye michakato yangu ya kiutafutaji/ ujasiliamali.
"Mapenzi ni maisha ya kila mja"
Nilimtambulisha kwa 'shilingi' yangu ya dhahabu kwa ridhaa na imani niliyokuwa nayo kwake, nilimpa cheo na kumuita mdogo wangu. Rafiki zangu wakawa dada na kaka zake, Shilingi yangu, akawa shem darling!
Woy, vilichukua muda basi? Nilikuwa na michakato fulani ya siri iliyohusisha utambulisho tofauti kabisa, (haikuwa haramu) ilinipa maokoto na kunifanya niwe na mapene ktk umri mdogo. Kigezo kikubwa cha ule mchongo ni usiri, kutokana na ukaribu na ujamaa bi shost alikuwa na mawasiliano na Shilingi yangu. Khee! Akaanza kunichongelea bana. Shilingi ikajazwa maneno. Ikawa inamlipa bibie anipeleleze, ukizingatia zilikuwa zile enzi za kubana mapaja angalau miaka miwili shilingi isifumbukie tunduni.
Bibie akamwambia, huyo mtu mfupi anakulaghai, kila siku anavaa anapendeza anaenda hoteli za kifahari na mapapaa. Mimi sina hili wala lile, kila leo nakumbana na maneno mapya kwenye kanga ya zamani.
Bwana weeh! Siku moja nikiwa kwenye windo langu la mapene, mkeka ukiwa mbioni kabisa kutiki, Shilingi yangu ikaingizana, ni baada ya kupewa dira iliyonyooka na mpelelezi wake aliyejua robo nzima ya maisha yangu. Aliingia bila ridhaa akidhani ni chumba cha mapumziko; bahati yake mbaya. Alijikuta akipigwa na bumbuwazi alipotazamwa na macho yaliyoziwamba nyuso zaidi ya ishirini zilizokuwa mkutanoni. Aliniona na mimi nilimuona; hasira zilinikwida baada ya shilingi kuropoka.
Alitamka neno baya, alitamka kwa hasira na chuki ya hali ya juu, maneno yote aliyoyasema yalimaanisha "Anagema tembo na linaishia kunywewa na wengine" Bibie hakuchoka. Aliendelea kunichongelea na kunisiginia kiatuni. Awali sikumdhania, na hata nilipoambiwa kuhusu unafki wa bibie sikusadiki asilani. Fitina zake zilipenya kiasi cha yeye kuitumikia shilingi yangu kijamii kabla yangu. Hapo aliishi katika himaya yangu kwa takribani mwaka na ushee! Tayari alikuwa na marafiki wengine, karibuni wote niliwajua na nilimpa onyo kuwahusu..
Sikio la kufa linasikia dawa basi! aliambatana na kunguru wenzake njiwa nikawa sina usemi. Wanasema karma ni halisi si ndio??. Shilingi yangu ilinyakuliwa na kuishia kutumika kama mpira wa danadana. Ilidundishwa kimatumizi, na mwishowe refa niliyeutazama mchezo nje ya uwanja nilitangaza matokeo. Mmoja wa mabinti wale watatu walioitumia shilingi iliyokuwa yangu kwa kuzungukana, alikuwa kakanyaga waya na mimi ndiye nilimsindikiza hospitali na kumpa ujasiri wa kuanza tiba ya kufubaza.
Haikunichukua muda shilingi ikaubaini ukweli. Mzunguko wa watu wanne ndani ya sulfuria moja. Kwangu haikujalisha hata kidogo maana tayari nilikuwa mbali na maisha yao. Mwisho wa ubaya ni aibu? Pengine ni kweli ila mwisho mzuri wa ubaya ni kulipa kwa kumuomba msamaha uliyemtendea.
Mzunguko wa dunia umenikutanisha naye. Kwa namna ile ile ya mkutano wetu wa kwanza. Mara hii alikuwa yeye na mtoto wake mdogo. Imani ileile iliyofanya niingie matatizoni nimeitumia kufanya mchakato wa kumuwezesha kufika nyumbani kwao.
KWANINI NIMEANDIKA?
Tulipokutana tulizungumza kidogo kuhusu maisha yetu ya sasa hivi. Kauli yake ya mwisho kabla ya kuagana niliielewa mno, alisema hivii;
"Eva naomba uniamini mimi, kuna mahali Mungu aliruhusu upite ili uwe tupa' ya kunolea vyuma vingine viwe na makali. Kila nikiwaza niliwezaje kukufanyia hila na unafki baada ya msaada wote ulionipatia, majibu nakosa. Labda ni darasa lililotakiwa kufikia watu kutoka kwenye uzoefu wako. Naomba waambie hao wadogo zetu na hata wakubwa zetu wenye mioyo midogo, malipo ya hila yana ladha chungu mno wasijaribu japo kuonja, wasimulie kisa changu na wewe waipate picha, usiniite rafiki sistahili hilo. Usinipe nafasi ya uadui kwenye hadithi yako maana itakuwa kubwa mno kulinganisha na malipo ninayoendelea kuyalipa hadi tamani ya uhai wangu. Nisamehe dada"
Misamiati yake migumu ilinipa funzo fulani. Hakuna aliye salama kwenye swala zima la kukoseana; hata mimi kuna namna, mahali fulani Mungu alinitumia kama mjumbe wa habari mbaya yenye funzo kubwa. Kikubwa TUSAMEHEANE"
TUJIFUNZE' kutokana na makosa yetu ya zamani na yale ya watu wengine.
Ukitendewa wema usioweza kuulipa, usilipe ubaya kisa tu unaumudu.
"Sijawahi kukushikilia, nilikusamehe kitambo kwa ajili ya usalama wa moyo na nafsi yangu" nilimpa jibu langu, nikamuaga kwa kumkumbatia kiroho safi kabisa.
Kwaheri ya kuonana.
✍ Malkia wa tabasamu.
Kungwi wa kisasa.
0742 6301 41