Tenda za serikali Miyeyusho, Takukuru mnatakiwa kuchunguza

Tenda za serikali Miyeyusho, Takukuru mnatakiwa kuchunguza

Selwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
583
Reaction score
590
Juzi katika kikao kimoja hoteli kubwa nchini nikakutana na mfanyabiashara mkubwa, nikamwambia mwanangu mbona hauongezi wigo wa biashara yako, akanijibu Tanzania haina biashara halali na ukafanikiwa. Doh nikastuka., tajiri akaendelea kuniambia Yeye ana duka kubwa ana mikataba na kampuni private na serikali ila ikija kwenye kulipwa ni mtafaruku.

Nikakumbuka ata mimi duka langu ka hardware nikipewa order na halmashauri sijui wizara ni kilio ulipwaji. Sasa nikashangaa hadi tajiri anapitia hiki hiki, leo nimeona kafunga duka lake (Mr Price) Hivi jamani Biashara hii nchi mnafanyaje? Kwani shida ni nini kwenye serikali na taasisi za serikali kulipa suppliers kwa muda? Ni kipindi kirefu nasikia wajenzi wanadai serikali, suppliers wanadai serikali, kwanini hamlipi kwa wakati? na nani awajibishwe kwa ulipwaji mmbovu wa serikali na taasisi zake kwa suppliers wao?

Naiona kama inatengenezea mazingira ya rushwa kwa lazima, kuna haja takukuru kuchunguza mifumo ya ulipwaji wa suppliers wa taasisi za serikali na wizara, halmashauri
 
Serikali imejengwa kwenye msingi wa rushwa na ufisadi
Hao wanaoidai serikali watoe ahadi yakutoa kitu kidogo uone kama hawajapewa pesa yao siku hiyo hiyo.
 
Serikali imejengwa kwenye msingi wa rushwa na ufisadi
Hao wanaoidai serikali watoe ahadi yakutoa kitu kidogo uone kama hawajapewa pesa yao siku hiyo hiyo.
Kuna miezi ya mwisho wa mwka wa fedha na mwanzo wa mwaka wa fedha,utajuta,hakuna kiumbe anakaba fedha za maskini kama serikali,na sasa yamewashinda kwa sasa hawana uwezo wowote na hali ni mbovu na hawana la kufanya sababu hawana la mbadala,very soon recession itatia timu,hawajui impact ya kukaba maskini wala kutumia kwa makini baada ya kukusanya,sisi tunakusanya alafu matajiri wanakopa na wao wanakopwa na maskini anafirsika na wao wanakopa Tena na maskini anapooza kwa stress na benki inakosa mteja na wateja wanapungua kila biashara hatimae fiesta ya diamond nayo inafifia na mwamposa anafulia na sadaka zinapungua na mashirika yanakosa pesa ya kutumia na wao wanakopa Tena kuhudumia mkopo, THE END
 
Kwani TAkukuru hao nao si ni serikali.....kwamba serikali ikajichunguze...ukifanya biashara na serikali tegemea kufilisika tuuu
 
Sasa ndugu unafanya biashara na watu wenye silaha za kivita ,utatoboa kweli?
Namkmbk jamaa mmj anahardware yy hana tenda za serikali hata moja. Anachokifanya, anakopesha wazabuni ila sharti aweke bond kitu km nyumba ,gari etc
 
Back
Top Bottom