Tendwa awaonya Kakobe, Sheikh Yahya
Ajiandaa kutunga sheria kali dhidi ya wanajimu
na Danson Kaijage, Dodoma
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amevunja ukimya na kuwajia juu baadhi ya viongozi na watabiri wa nyota ambao wamekuwa wakiwatishia wapiga kura, kwa kuwalisha mafundisho yasiyo sahihi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, kuhusu suala la wagombea kurudisha fomu za gharama ya uchaguzi kwa wakati, Tendwa alisema watu hao wamekuwa wakitaka kuhatarisha usalama.
Aliwataja viongozi hao kuwa ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship na mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, kuwa ni watu hatari, ambao wanaweza kuleta fujo ndani ya nchi kutokana na mafundisho yao pamoja na utabiri usio kuwa na msingi wowote.
Alisema kitendo cha Askofu Kakobe kutoa elimu ya uraia kanisani kwake, kinaonyesha wazi amejiingiza katika kampeni za kisiasa na kusahau kazi yake ya kuwahudumia watu wake neno la kiroho.
Alisema viongozi wa dini wanatakiwa kutoa elimu ya kiroho ambayo itawapa mwanga waumini wao, ili waepukane na maovu na si kugeuza madhabahu kuwa uwanja wa siasa.
Alisema kitendo cha Sheikh Yahya kutoa utabiri wake kupitia kipindi chake cha nyota kinachoonyeshwa katika moja ya vituo vya televisheni jijini Dar es Salaam, kinaonyesha wazi kukipigia kampeni moja ya chama kati ya vyama viwili vyenye nguvu, jambo ambalo ni mwelekeo wa uvunjifu wa amani.
Alisema kutokana na tabia ambazo zinaonekana kukua kati ya makundi ya dini na siasa, kuna kila sababu ya kuangalia upya sheria ambayo itaweza kudhibiti viongozi wa dini kutojiingiza katika siasa ama kuwadhibiti watu kama Sheikh Yahya, ili usomaji wa nyota uwe kwa faida yake na si kuwachanganya wananchi.
Akionekana kuwa mkali, Tendwa aliponda baadhi ya taasisi ambazo zimekuwa zikitoa taarifa za mgombea gani anaongoza kupendwa.
Bila kutaja taasisi hizo, hivi karibu Kampuni ya utafiti ya Synovet ilitoa matokeo ambayo yanaonyesha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete, anaongoza kwa kupendwa.
Nina shangazwa na taasisi zinazoendesha kura za maoni juu ya mwenendo mzima wa hali ya kisiasa na kutoa mwelekeo wa ushindi katika vyama vya huu ni uchochezi kwa wananchi, alisema Tendwa.
Akizungumzia urudishaji wa fomu za gharama za uchaguzi, alisema wagombea wote wanatakiwa kurudisha fomu hizo ili zifanyiwe uhakiki.
Alisema mgombea ambaye atabainika hajarudisha fomu hiyo ataenguliwa katika uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kupewa adhabu ya kutogombea nafasi yoyote katika uchaguzi wa mwaka 2015. Alisema pamoja na hilo, baada ya uchaguzi wagombea watapewa siku 60 ili kupeleka vielelezo vya mapato na matumizi kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ili kubaini iwapo gharama zilizowasilishwa zimetumika kama ilivyokusudiwa. Alisema iwapo sheria hiyo itaonekana imekiukwa, kwa kuonyesha mgombea ametumia pesa nyingi zaidi, atalazimika kutoa maelezo na iwapo maelezo yake hayatakubaliwa, atafutiwa matokeo.
source TANZANIA DAIMA 03/10/2010