Facts1
JF-Expert Member
- Dec 23, 2009
- 307
- 28
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa, ametetea hatua ya mgombea wa kiti cha Urais kupitia tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete, kuhusu kufanya mikutano ya kampeni zaidi ya saa 12 jioni na kueleza kuwa kuanzia sasa wamekubaliana mwisho wa kampeni ni saa moja usiku.
"Ni kweli kwamba muda wa mwisho wa kampeni huko nyumba ulikuwa ni saa 12 jioni, lakini muda huo ulikuwa na tofauti sana katika kumaliza mikutano katika baadhi ya maeneo kama ya Mkoa wa Kigoma na kule Ngara ambako saa 12 jioni, bado ni mapema sana,"alisema Tendwa.
Tendwa alisema kwa msingi huo, si makosa sasa kwa mgombea wa CCM, (Kikwete) kuhutubia zaidi ya saa 12 kama ambavyo imetokea katika mikutano yake ya hivi karibuni mkoani Arusha na Manyara.
Hata hivyo alipoulizwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (Nec) Jaji Lewis Makame alisema, tume haijapata taarifa hizo na kuwa bado wanaamini kuwa muda wa mwisho wa kampeni ni saa 12 jioni.
"Ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako taarifa hizo, kwani kayasemea wapi hayo," alihoji Jaji Makame.
Alisema Nec itafuatilia taarifa hizo na kwamba ikithibitisha, itatoa tamko lake.
My take: Tanzania ni ya ajabu kweli sheria zinapindishwa kum-fit mtu na si mtu ku-fit sheria kwa hali hii hatufiki tunakotarajia.