Awali ya yote nawashukuru JamiiForums kwa kutoa fursa hii ya kuwasilisha mawazo kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu hususani kwa sisi vijana, ambapo tunapata nafasi ya kuwasilisha mawazo yetu. Si kila takataka ni takataka.
Tunawezaje kujua hili, ni kwa kutenga takataka wakati wa ukusanyaji.
Binafsi naweza kusema Mfumo wa ukusanyaji taka tulionao sio mbaya ushirikiano wa serekali na watu binafsi ni jambo zuri. Hasa kwenye mambo yanayonufaisha jamii zetu kama afya, elimu, utunzaji mazingira nk.
Ingependeza wakusanyaji kukuta taka tayari zimetengwa kwa makundi taka kavu, taka zenye unyevu, taka zinazochomeka, taka zisizochomeka n.k
Hii itafanya kuwe na urahisi wa kupata taka zinazoweza kutumika tena. Pia itaongeza fursa maana kwa kutenganisha taka itahitajika mikono ya ziada kuhakikisha kila kundi la taka linafika mahali husika kufanyiwa taratibu husika za kuzitokomeza, haina maana taka za kuchoma kuwepo dampo/jalalani au taka zinazoweza kutumika tena au taka zinazotokana na vyakula zote hizi zinaweza kutokomezwa kwa namna zingine kabisa.
Tunawezaje kufanya hivyo basi.
Kukiwepo na mfumo wa ukusanyaji taka kwa kutengisha kuanzia daraja la chini kabisa yani manyumbani, ofisi na sehemu za biashara mfano.
Kuwepo kwa mifuko rasmi ya taka inayotofautiana rangi, 🟨(njano)taka zinazoweza kutumika tena(recycle), ⬛taka zakuchoma, 🟩(kijani)taka zinazotokana na chakula.
Itapunguza mrundikano wa taka kwenye madampo na hatutolazimika kutenga maeneo makubwa au ata maeneo mapya ya majalala/madampo.
Hatuwezi kurudisha muda nyuma ila hatima ya vizazi vya baadae ipo mikononi mwetu tunaweza kufanya jambo sasa tjkayatunza mazingira yetu, kufungua fursa nyingi zaidi na hata kukngeza ajira tele ndani ya muda mchache.
Mazingira yetu kesho yetu tuyatunze yatutunze, vizazi vijavyo wapate kufurahia mazingira safi. Sisi ndo kizazi cha kufanya amani na mazingira.

Upvote
0