Tengeneza kitotolesho cha kuku mwenyewe

Tengeneza kitotolesho cha kuku mwenyewe

washeby

Member
Joined
May 28, 2015
Posts
32
Reaction score
4
Mahitaji
Boksi, bakuli la maji, bulb, holder na themometer.

Jinsi ya kutengeneza
Toboa boksi mduara wa kutosha kufit bulb, weka mayai, bakuli la maji kwa ajili ya kutengeneza unyevu na mwisho weka thermometa.
Unganisha umeme na kaa nusu saa, hakikisha kipimo chako kinasoma 38c geuza mayai kila baada ya masaa manane kwa muda wa siku 17-19.
Joto likizidi waweza funua boks ili kupunguza joto na kisha funika tena.
 
Boksi la a in a fani mkuu?? Na moangilio wa hyo vitu unakuaje??? Ungeweka na picha ingekua poa zaidi
 
Safi kabisa mkt, kuna vitu huja vielezea vizur,
1. balb ya watt ngapi?
2. box unalo ongelea ni haya ya kawaida makubwa? kama ya bohari ya dawa?
3. maji kiasi gani?
4.vipi usiku, lazima uamke kila siku kugeuza?
5.nitayaweka ktk tray au hata yakibebana?
6.Vipi umeme ukikatika siku nzima unafanyaje?
asante kwa darasa.
 
Kakopi sehemu kaja ku paste kakimbia mweee. Lakini ni daralasa nzuri ila kwa umeme wetu lazima upate hasara ya mayai.
 
Kakopi sehemu kaja ku paste kakimbia mweee. Lakini ni daralasa nzuri ila kwa umeme wetu lazima upate hasara ya mayai.

Kabla sijapata ajira niliwahi kufikiria alivyo fanya mleta mada, changamoto ikawa jinsi ya kupata mayai ambmyo ni mazima, yaani yawe hayajatikiswa na hayaja dondokewa maji, nikashindwa, nikawaza kuzunguka ktk kaya mwenyewe na kukusanya pia nikahisi nitafikiriwa vibaya kua nitashawishi watoto kuiba mayai na kuniuzia nikaamua kuacha. hivyo kanikumbusha mbali sana
 
Back
Top Bottom