Tengua - teua ni danganya toto tu! Hazina tija yoyote ile

Eti washauri wanamshauri vibaya!!!

Lame.
 
Nimeshuhudia watu wakijenga majumba yakifahari kutokana na mapesa ya kuhamishana hovyo!! Nadhani kunamchezo usio safi unafanyika ili watu fulani waweze kujiingizia mihela kiharamia.
CAG akague uhamisho umeligharimu taifa kiasi gani kwa miaka hii mitatu tuu ili amshauri mama msafiri ubaya wahaya afanyayo!!! 🤣🤣(Kesho afukuzwe kazi).
SWALI,mbona mawaziri waki Zenji hawatumbuliwii?? Huyu wa UCHUKUZI amesababisha hasara kibao kupitia TRC,ATCL nk. lakini anadunda tuu kazini!!
Yaani wadada wawili wakizenji Sa100 na Yunusu wanatikisa mabichwa ya viongozi Kila wakiamka wanatetemeka mkeka usijetoka!! Aibu saana hii nchi😞
 
Hivi hao watu wanaotenguliwa wanalipa ela za uhamisho, au wanahamishwa tu
 
Naiita CCM ni recycle bin sababu kila siku inaingia kwenye "PIPA la taka" na kuona "takataka" gani waliiweka mle na wairejeshe kwenye desktop iweze kuonekana.

Hizo "takataka" zinazoibuliwa kila siku hakuna zinazofanya zaidi ya kujigamba wao ni Watoto wa mjini.
 
Wewe ni Makonda uliechangamka
 
Meli inayoendeshwa ni mbovu na imetoboka, na hata Manahodha wa meli nao pia ni wabovu, kwa hiyo suala la Meli kuzama liko pale pale hata kama watabadilishwa Manahodha wa meli mara milioni moja, wala haitasaidia kitu.
Suluhisho pekee ni kutengeneza/kuunda meli mpya na kuwaajiri Manahodha wapya wenye utaalamu na ujuzi unaofaa wa kuendesha hiyo meli mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…