Terehe 14 Disemba, 2021, DPP atawasilisha Nolle kesi ya akina Mbowe?

Terehe 14 Disemba, 2021, DPP atawasilisha Nolle kesi ya akina Mbowe?

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Mawakili wa Serikali waliomba muda Zaidi kuandaa Maelezo yao ya maandishi kwani Mh. Jaji mwenyewe alikuwa tayari kutoa uamuzi wake kesho. Baadhi ya waliowasikia Wanasheria wa Serikali walivyotoka jana wanadai kuwa iwapo uamuzi utatoka kuonesha Mtuhumiwa Ling'wenya aliteswa basi Serikali itaendelea kuumbuka.

Kutokana na hali ilivyo na kwa dalili walizoziona kwenye kesi ndogo iliyokamilika kusikilizwa jana wameshauriana wawasilishe ombi la "Nolle" ili kesi isiendelee na watafute namna ingine ya kujisafisha.

Jana hiyo Mawakili wa Serikali walikuwa desparate sana wakiona kuwa wamepewa kesi ambayo imeanza kuwachafua katika jamii yetu. Walisikika wakimwomba Kiongozi wao Kidando aakutanishe kwa DPP kujadili hilo.
 
Hawa makomandoo wa JWTZ wameteswa sana aisee, mateso makali kudhalilishaji wa ubinadamu wao, hata JWTZ wenzao wasifurahie kitendo hiki kabisa kabisa.

Hii kesi ifutwe tu, maana inaleta simanzi kubwa miongoni mwa watanzania.
 
Hawa makomandoo wa JWTZ wameteswa sana aisee, mateso makali kudhalilishaji wa ubinadamu wao, hata JWTZ wenzao wasifurahie kitendo hiki kabisa kabisa. Hii kesi ifutwe tu, maana inaleta simanzi kubwa miongoni mwa watanzania.
Inazidi kuibua chuki kati ya hizi taasisi na kati yao na wananchi pia. Sio afya kwa mustakabal wa taifa.
 
X-mas na mwaka mpya mazee, kila mwezi wanaigiziwa 3,600,000 nje na mishahara yao, usafiri bure, stationery n.k ni zaidi ya mgodi mkuu

Nakuelewa sana mkuu. Ila kwa hii kesi wasipochukua tahadhari, wajiandae kwa kitu kizito. Mambo yameparanganyika sana. Wananchi wamehamaki, chuki ikiendelea namna hii hapatakua na utulivu.
 
Back
Top Bottom