Humu kuna baadhi ya mambo yameongelewa ambayo ni ukweli kabisa na yanafanya ushuhuda huu uwe wa ukweli kabisa, ukiangalia hizi teknolojia zinavyovumbuliwa kwa kasi kipindi hiki ni ngumu kusema ni binadamu ndio anavumbua awe mzungu,mchina n.k jibu ni hapana.
Kuna viumbe ambavyo vinawapatia hii teknolojia taratibu taratibu kutoka kwenye kiwango cha chini mpaka cha juu kabisa ijapokua zipo teknolojia za kutisha ambazo binadamu hajapewa. Ukija kwenye hizi dini zetu ndio usiseme kuna uhuni mtupu unaendelea sio ukristo(roman,urutherani,usabato,ulokole n.k) pamoja na uislamu humo kwenye hizi dini ni uhuni mtupu na nikweli kabisa watu wengi niwadini hawaishi maisha halisi ya kikristo na kiislamu kabisa.
Wengi wanashindwa kujua yakwamba dini ni utamaduni tu.bila kujua hapa ndio shetani anapochukua pointi sababu vitabu vitakatifu vyenyewe kama biblia na quran alishavichakachua kabisa ili mafundisho yake yaendane na falsafa na muongozo anaoutaka yeye. Na hapa nikama mtu anawategemea viongozi wa dini basi imekula kwake.
Mie naamini kumjua MUNGU inabidi kujitoa kwelikweli nakuwa na nia thabiti ndani yako na MUNGU atajifunua na kukupa muongozo mzuri wa kuishi maisha matakatifu. Sababu hata huu mfumo wetu wa maisha ni mfumo feki ambao MUNGU akutupangia tuishi.