TET: Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum hawajasahaulika katika mifumo ya Kujifunza

TET: Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum hawajasahaulika katika mifumo ya Kujifunza

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Anselmo Komba, amesema kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kuweka mazingira jumuishi ya kujifunza kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kuhakikisha wanapata vifaa na nyenzo sahihi za kujifunzia na kufundishia.
65465b56-6193-43b9-8524-cc22387762b2.jpeg
Mafanikio ya Elimu Jumuishi

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya TET, Dkt. Aneth amesema kuwa juhudi mbalimbali zimechukuliwa ili kuondoa tofauti katika upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi wenye changamoto za ulemavu. Alieleza kuwa hapo awali wanafunzi hao walilazimika kuwa na wasaidizi maalum, lakini sasa changamoto nyingi zimepatiwa ufumbuzi.

Vitabu Maalum kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji

Dkt. Aneth amesema kuwa TET imefanikiwa kutafsiri vitabu vyote vya kiada katika maandishi yaliyokuzwa kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu, pamoja na vitabu vya maandishi ya Brell kwa wanafunzi wasioona.

“Tumefanikiwa kutafsiri vitabu vyote vya kiada katika maandishi ya Brell na yaliyokuzwa kwa matumizi ya wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu mtawalia,” amesema Dkt. Aneth.
b1f6d904-972b-4217-983a-7094f8678b55.jpeg
Ameongeza kuwa vitabu vya kiada vya masomo ya Sayansi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa macho vimechapishwa na kusambazwa kwa uwiano wa kitabu kimoja kwa kila mwanafunzi (1:1), huku vitabu vya masomo mengine vikisambazwa kwa uwiano wa 1:3.

Mtaala na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Dkt. Aneth pia amesema kuwa katika maboresho ya mitaala, wamejumuisha vipengele muhimu vinavyoendana na mahitaji ya sasa. Aidha, taasisi hiyo imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mitaala hiyo kwa karibu.

Ameeleza kuwa TET imeanza kuchukua hatua za kuhimiza matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji, ikiwemo mpango wa kugawa zaidi ya kompyuta 16,000 kwa shule za sekondari katika mikoa 10, kwa ngazi ya kidato cha tano.

Majukwaa ya Kujifunzia na Changamoto za Internet
728c822f-4d71-437f-97f0-b1fc3e05528c.jpeg
TET pia imeandaa majukwaa maalum ya kujifunzia kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali. Hata hivyo, changamoto ya gharama za huduma ya intaneti imeelezwa kuwa kikwazo kikuu kinachokwamisha utekelezaji wa majukwaa hayo kwa ufanisi.

“Tunaendelea kufanya mazungumzo na wadau wa huduma ya intaneti ili kupunguza gharama na kuwezesha utekelezaji bora wa mpango huu,” aliongeza Dkt. Aneth.
 
Back
Top Bottom