Tetemeko lenye ukubwa wa 7.0 laipiga Uturuki, 14 wafariki

Tetemeko lenye ukubwa wa 7.0 laipiga Uturuki, 14 wafariki

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105
1604073605745.png

Tetemeko la Ardhi lililotokea mchana wa Ijumaa ya tarehe 30 Octoba 2020 katika ukanda wa Bahari ya Aegean limeharibu miundombinu katika miji ya pwani.

Watu katika Mji uliopo Magharibi mwa Uturuki , Izmir wamekusanyika katika mitaa baada ya kuyakimbia majengo yao wakitafuta usalama. Meya wa mji wa Izmir amethibitisha kuwa takribani majengo 20 yameharibiwa katika Mji huo.

Taarifa zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Suleyman Soylu kupitia mtandao wa Twitter ni kuwa Miji mingine iliyoharibiwa na Tetemeko hilo ni Bornova, Bayrakli.

Aidha Waziri Soylu ameongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea katika eneo hilo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa takribani watu wanne (4) wamefariki huku 120 wakiwa wamejeruhiwa kufuatia Tetemeko hilo.

Idadi ya waliofariki kwenye Tetemeko hilo yaongezeka mpaka kufikia 14, na majeruhi 400.

UPDATE: WALIOFARIKI KATIKA TETEMEKO UTURUKI WAFIKIA 24, ZAIDI YA 800 WAJERUHIWA

Tetemeko la ardhi lililotokea jana limepelekea vifo vya watu 24 hadi sasa huku wengine takriban 804 wakijeruhiwa

Rais Recep Tayyip Erdogan amesema kati ya waliojeruhiwa, watano wamefanyiwa upasuaji na nane wapo kitengo cha wagonjwa mahututi

Aidha, tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 7.0 wa kipimo cha Richa pia limeikumba Ugiriki na kupelekea vifo vya vijana wawili ambao waliangukiwa na ukuta

Msichana wa miaka 3 aokolewa akiwa hai baada ya kukaa chini ya kifusi kwa saa 65.

Msichana aliyetambuwa kwa jina la Elif Perincek, ameokolewa asubuhi ya leo Jumatatu ya tarehe 2

Waziri wa Afya wa Utururki Fahrettin Koca amesema kuwa Mama wa Perincek pamoja na watoto wengine wawili wameokolewa leo asubuhi , ila ndugu mmoja alikuwa kashafariki dunia.

Na saa kadhaa nyuma Msichana mwingine wa miaka 14 aliokolewa chini ya kifusi akiwa hai baada ya kukaa zaidi ya saa 58
 
Back
Top Bottom