Tetesi: Airtel kubadilika tena!!!

Tetesi: Airtel kubadilika tena!!!

steering

Member
Joined
Nov 28, 2011
Posts
71
Reaction score
12
Sasa ni wazi kuwa iliyokuwa kampuni ya Celtel, ikawa zain na sasa airtel imeogewa kwa kujibadilisha majina. siku si nyingi itakuwa rasmi chini ya makaburu hivyo kuitwa Orange Tanzania. chanzo cha kuaminika kinachofanya ndani ya company hiyo kimedokeza wafanyakaz wanajiandaa kimawazo kubadilika na kuzoea "orange Tanzania" kwa usalama wake jina linahifadhiwa
 
Huu ni mkakati wanaouendeleza wa kukwepa kulipa kodi,
Nasikia wawekezaji hupewa miaka mitano ya majaribio bila kulipa kodi, ila miaka mitano ikiisha ndo wanaanza kulipa kodi.
Sasa kinachoonekana hapa ni kukwepa kulipa kodi na kubadili jina wakijidai wamefilisika na kumuuzia kampuni mtu mwingine.
 
Hizo si biashara kama biashara nyingine? sioni cha ajabu, hapo sheria mpya ya "capital gain" iko upande wetu, kama imeuzwa, lakini inawezeekaana tu kuwa wanachukuwa "franchise" ili wafanyiwe menejimenti na orange kwani ni wazoefu zaidi wa Africa.

Sioni ubaya wowote.
 
Waungwana kama imeuzwa sidhani kama kuna tatizo. Serikali itachukua capital gain tax na new investor anachukua new team.

Kumbukeni most of this deals kuna watu wameweka pesa zao and they need a dividend or capital gain. Sasa muda wa cash ukifika watu wana exit hiyo ni normal sana.
 
Hizo si biashara kama biashara nyingine? sioni cha ajabu, hapo sheria mpya ya "capital gain" iko upande wetu, kama imeuzwa, lakini inawezeekaana tu kuwa wanachukuwa "franchise" ili wafanyiwe menejimenti na orange kwani ni wazoefu zaidi wa Africa.

Sioni ubaya wowote.

Nakuunga mkono mkuu. Tunachohitaji ni huduma bora na gharama nafuu, kubadilika kwa jina hakuniathiri chochote.
 
Dah haya no wonder why Tanzania is still poor.
Tuanze na Serena ishabadilishwa majina kibao.

Kilimanjaro kempsk sa hii inaitwa Hyat regency (kwa maandish madogo) THE KILIMANJARO hapo hawajabilisha maana ni ujanja tu huo.

Airtel.. ilianza kama celtel ikaja zain

tuje tigo. buzz mobitel

fly 540
sasa ni fastjet.

Hao wote kila wakibadilisha tunawapa tax holiday almost 5 years eti wajaribu biashara kama wenzao wameshindwa si waweke biashara nyingine hivi tutakua wajinga mpaka lini kuvumilia hii hali? si wazungu wanatucheka huu mradi ushakuwa wa wachache sasa.
 
Huu ni mkakati wanaouendeleza wa kukwepa kulipa kodi,
Nasikia wawekezaji hupewa miaka mitano ya majaribio bila kulipa kodi, ila miaka mitano ikiisha ndo wanaanza kulipa kodi.
Sasa kinachoonekana hapa ni kukwepa kulipa kodi na kubadili jina wakijidai wamefilisika na kumuuzia kampuni mtu mwingine.

Watanzania tumezidi "kusikia"
Tusome kidogo hata sheria ya kodi ya mapato, Tanzani Investment Act..etc
 
nanukuu....... " WATANZANIA TUACHE WIVU WA KIJINGA KWA WAWEKEZAJI"........ mwisho wa kunukuu
 
Dah haya no wonder why Tanzania is still poor.
Tuanze na Serena ishabadilishwa majina kibao.

Kilimanjaro kempsk sa hii inaitwa Hyat regency (kwa maandish madogo) THE KILIMANJARO hapo hawajabilisha maana ni ujanja tu huo.

Airtel.. ilianza kama celtel ikaja zain

tuje tigo. buzz mobitel

fly 540
sasa ni fastjet.

Hao wote kila wakibadilisha tunawapa tax holiday almost 5 years eti wajaribu biashara kama wenzao wameshindwa si waweke biashara nyingine hivi tutakua wajinga mpaka lini kuvumilia hii hali? si wazungu wanatucheka huu mradi ushakuwa wa wachache sasa.
Hata BOFLO wa JF alibadili jina na wala hamkushangaa, itakuwa hao...
 
hatuwezi kuwagomea kama yanga walivyogomea nembo nyekundu za voda?
 
Bora wabadili.......at least tutaweza kuroam mbali zaidi ya Asia .....khaaaaa
 
Naona kuna haja ya kuweka sheria kampuni ikishatimiza miaka mitano ata ibadilishe majina mara kumi ni kunyuka kodi tuu maana sasa huu uhuni!
 
Hizo si biashara kama
biashara nyingine? sioni cha ajabu, hapo sheria mpya ya "capital gain"
iko upande wetu, kama imeuzwa, lakini inawezeekaana tu kuwa wanachukuwa
"franchise" ili wafanyiwe menejimenti na orange kwani ni wazoefu zaidi
wa Africa.

Sioni ubaya wowote.

Capital gain? je, kama imeuzwa kwa "hasara"...
 
Haitazamwi bei iliyouzwa inatazamwa thamani ya hiyo kampuni iliyouzwa, ndiyo maana inaitwa "Capital Gain".
 
Back
Top Bottom