Tetesi: Goal keeper wa ZANACO kuja Simba

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Goal Keeper wa ZANACO Toaster Nsabata, wiki hii anatua msimbazi kuja kufanya majaribio.

Wanasimba maoni yenu.

 
Ili kuwa na timu bora yenye ushindani, unahitaji wachezaji wazuri(bora)
 
Simba haina tatizo la kipa.

Labda kama ungetabiri kuwa Prince Dube anakuja Msimbazi kumpa ushindani Boko.

Abdi Banda anarejea tena kumpa ushindani Mohamed Hussein, Nafasi ya Fraga tayari ishapata kifaa, Bado beki wa kulia Kapombe akiumia yule Dogo toka Lipuli sijaona akipewa nafasi.

Tatizo kubwa la wachezaji wengi wa Simba wanacheza taratibu na hawajitumi kama ilivyo kwa Luis Konde Boy au kama ilivyo kwa wachezaji wote wa Yanga.
 
It's a welcome news. Manula wetu anatupa pressure kwenye mipira ya juu inayopigwa kutoka mbali.
 
Usajili wa kiboya tu usiozingatia mahitaji.
simba haina deep mildfielder mwenye nishati ya kutosha anayecheza kwa maelekezo.
akina mkude wako driven na majukwaa.

Lakini, zipo nchi misiri ikiwemo hawa-import makipa toka nje kwa mujibu wa sheria zao.
nafikiri ktk mataifa mengi demand ya makipa ndogo mno.na makipa wabovu duniani ni wachache ukilinganisha na positions nyingne uwanjan
na ndio maana bei zao huwa ni ndogo.

Simba ikumbuke ina nafasi 10 tu za nyota wa kigeni.ukisajir huyo kipa utalazimika kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni il idadi ibaki ileile kikanuni
 
Tatizo kubwa la timu yetu Simba...ni nafasi ya ushambuliaji na kiungo mkabaji... Bocco ana pancha hivyo anacheza kwa tafadhari Sana asiumie....Kagere ni mzuri akiwa ndani ya box.... akitoka nje ya box hana madhara....Mugalu huyu nadhani tumeingia cha kike....ni majeruhi...lakini naye pia ni anakuwa mzuri akiwa kwenye box...watu wa usajiri wapambane watafute mshabuliaji kijana..mpambanaji kama Konde boy....kuna Kipindi ilisikika tunamchukua yule mshabuliaji wa Nkana Water bwalya...yule jamaa angetufaa Sana.
 
Huyo Golikipa siyo hitaji la Simba kwa sasa, Simba kwa sasa inataka Mshambuliaji Mahiri mithili ya Hertier Makambo au Makusu au Walter Bwalya au Lusajo. Mbona Viongozi mnatutaka maneno manenoooo. Kwa taarifa yenu kutokana na mwenendo mbovu wa timu Idadi ya mashabiki Uwanjani imekuwa hafifu mnoo.
Iweje Usajili mpya woooote wa akina Bwalya, Morrison, Mugalu, Onyango nk nk wooote hawana namba kwenye First Eleven??? Mnamaanisha nini Viongozi? So paining lkn tambueni kuna Mashabiki tunatoa pessa ili timu iendelee kupata sapoti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…