Tetesi huanza na minong'ono

Tetesi huanza na minong'ono

Tetesi huanza na minong'ono.. Hiyo minong'ono ikikoma huwa tetesi na tetesi zikikoma huwa breaking news.

Dunia ya sasa iko uchi kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia. Dunia haina siri tena!
Unafanya jambo gizani. Tena giza totoro kabisa lakini unakuja kushangaa jambo hilo linakuja kuwekwa upenuni peupe kwa picha safi kabisa

Kuficha taarifa yoyote kubwa inayoihusu Jamii haisaidii chochote. Tunaweza kafanya hivyo kwa lengo maalum na sababu maalum lakini kwa dunia hii ya sasa. Taarifa zinaweza kuvuja zenyewe bila hata kuvujishwa na yoyote yule

Kuna madhara makubwa kwenye taarifa kuvuja zenyewe. Maana ni sawa na bomba la maji lililopasuka na kuvujisha maji barabarani.

Yale maji hayana mwenyewe.. Yeyote anaweza kuyatumia vyovyote

Taarifa zinazovuja zenyewe hurembwa, hutiwa nakshi na kuongezewa vikolombwezo vya kila aina kulingana na mahitaji ya mlengwa!

Hakuna siri ya mtu moja duniani.. Ni fikra finyu kuruhusu minong'ono itawale kuliko kuweka wazi.. Akili ya binadamu ni kitu kisichozuilika.. Ukiibania taarifa unaiongezea udadisi na mshawasha wa kutaka kujua zaidi.. Kujua kulikoni...

Minong'ono ya Msechu kujiandaa kuingia studio ni uzushi usiofaa kupewa kipaza sauti
NIMEPITIA COMMENTS NYINGI NIMEGUNDUA BINADAMU HUA INAFIKA POINT ANABADILIKA NA KUWA MBAYA ZAIDI YA KIUMBE CHOCHOTE HATARI UNACHOWEZA KUWA UNAKIFAHAMU HAPA ULIMWENGUNI.

ALL IN ALL MUNGU IKIKUPENDEZA SHUSHA GHARIKA LAKO WATU WOTE+ KIZIMWORK WAKUFAHAMU.
 
Wewe ni mzushi kwa kuwa umenisingizia mimi uzushi wakati wewe ndie mzushi mkubwa kwa kukataa kwa makusudi au kujifanya huoni ushahidi uliomo humu uzini kwamba wakristo wanafurahi na wanaombea muislamu afe tena hasa muislamu rais wa inchi,

Lakini kikubwa kuliko yote ni kuthibitika kwako leo kwamba wewe una dini na dini yako ni ukristo, na ndio maana post imekugusa sana na umeimaind kweli kweli

Kidogo kidogo tu itajulikana
Mjomba mzushi
Hapa tunazungumzia kifo cha BINADAMU mwenzetu hatuzungumzii dini acha kuchanganya mambo nyie ndo shuleni mlikuwa mnashika mikia na kukariri kwenu
 
Screenshot_20241110_083301_X.jpg
 
Mk
Mkuu ukosefu wa ajira katika jamii ya Tanzania ndo chanzo cha tetesi na minong'ono, hu uzi wako watu watatunga mengi na kuhama mada kwasbb wengi hupenda taarifa mbaya kwa wenzetu......yangu ni macho hu uzi unaishia pabaya tuna roho za kishetani, kwasbb lilitokea kwa JPM wengi hutamani limkute na mgine ila Mungu hafuati matakua ya watu, Mama bado yupo mpaka pale mungu atakapo penda kadari yake ifike.
uu kuna ile law inasema "to every action there is equal and opposite reaction".kwa sasaiv haya mambo ya watu wakawaida kuwatakia mabaya viongoz ni tabia mbaya saana saana,ila kuyazuia ni vigumu saana.Hii ni kutokana na dhana ya baadhi au wataz walio wengi kuamin kuwa serikali inahusika ktk matukia ya kuumizwa,kupotea au kuuawa kwa baadhi ya watu.Sasa wewe unadhan watu wa karibu au wotz walioguswa na wahanga hao watawawazia nini hao wanaowadhania kuwa ni wahusika !?.
Ushauri wangu hata kama kunasababu zozote za kiusalama,kisiasa au sabab binafsi zisizozuilika zinazo pelekea serikali kuhusishwa ktk baadhi ya matukio ya kuumia kwa baadhi ya watu basi liingaliwe katika weledi wa hali ya juu sana na uliotukuka kwa maslahi mapana ya umoja wa kitaifa kuanzia viongozi hadi raia wa kawaida wa itikadi zote.
 
🥺🤔🙇🏿‍♂🙌🏿Kuzungumza ukweli wa kujenga kwa mamlaka sio kuwadharau, badala yake ni kuwa na heshima na kusaidia. Kuwaambia mamlaka kile wanachotaka kusikia hata tunapojua hakina msaada kwao ni uhalifu.

20:54 13 Mei 24 Maoni 6,836View attachment 3148180
Ndio ndio kwamba "mki print pesa mtaikosea benki ya Dunia na Sheria sake,msifanye hivyo!wao wakafanya na kukupuuza ndio ikawa au!!?

Najiuliza tu,ukiwa mkweli kuliko serikali unakua matatani!
 
Habari na michango mingi ya watu kwenye huu uzi uwe kipimo cha kujitathmini pale unapopewa dhamana ya kuongoza wengine.

Kwa Afrika viongozi wengi wanageuka kuwa watawala badala ya viongozi inayopelekea ukengeufu.

Kikubwa viongozi watende haki kama wajibu na sio mpaka ujikombekombe au uwe chawa.
 
Back
Top Bottom