Tetesi: Kocha msaidizi wa Simba Mssoud Djuma afungashiwa virago

Kanali G

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2013
Posts
9,898
Reaction score
14,413
Kuna tetesi nimezisikia kwenye vijiwe kuwa kocha msaidizi wa Simba Mrundi Masoud Djuma Mkataba wake umesitishwa, mdau mwenye taarifa zaidi atiririke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli, hakukamilisha taratibu za Uhamiaji/kibali cha kazi...ni sawa na yule Ceo wa vodacom TZ aliyekosa iyo kazi kisa hajapewa kibali. Hamna ujanja janja tena awaumu hii.
 
Naona Ndala umekuja Na Speed si Ya Kawaida Kuleta Udakau?
Umeambiwa Akiondoka Masud Djuma Ndiyo Mwisho Wa Simba Nini?
 
Hawa Vyura FC Kwa Umbea hawawezrkani! Sasa Yule Aliyekuepo Katika Benchi la Simba Leo vs Mbeya City alikuwa Masud gani?
Hebu shuhulikieni Kukichangia Kigenge Chenu angalau Wachezaji wapate Kula Mboga na sio Kukomaa na Umbea zidi ya Matajiri Wa Msimbazi.
 
Yanga Ndiyo Zaidi Wanaoharibu CV za Makocha Manake Ni aibu Katika CV ya Kocha Kuandikwa Kipengele Cha Club Ombaomba Mitandaoni.
Kipindi yanga anafululizà kuchua makombe simba mlifukuza makocha wangap na kuwaaribia cv zao? Mmojawapo yule wa Gormahia sasa hivi
 
Simba watakua wamefanya kosa kubwa sana kama kweli watakua wamemuacha au wanampango wa kuachana na Masud Djuma

Makocha wa kizungu wanaokuja kutafuta ajira katika nchi kama zetu hasa kwa vilabu vinavyobangaiza mapato kama Simba, Yanga n.k hua ni wa kiwango cha kawaida sana ila wanabebwa na rangi yao na ushamba wa sisis waswahili

Djuma anaujua mpira, anawajua wachezaji, anaongea lugha yao na anafahamu mazingira ya uchezaji ya kiafrika na juu ya yote kaonyesha matunda yake katika kipindi chote alipokua anahudumu kama kocha mkuu
 
Kawaida, habari uanza kama tetesi. Lisemwalo lipo. Naishia hapoo.

 
Masudi mtovu wa nidhamu anashinda bar na wachezaji wanalewa mpaka asubuhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…